Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Yeremia 51:9 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

9 Tungependa kuuponya Babeli, Lakini haukuponyeka; Mwacheni, nasi twendeni zetu, Kila mtu hata nchi yake mwenyewe; Maana hukumu yake inafika hata mbinguni, Nayo imeinuliwa kufikia mawinguni.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 Tulijaribu kuuponya Babuloni, lakini hauwezi kuponywa. Uacheni, twendeni zetu, kila mmoja katika nchi yake, maana hukumu yake ni kuu mno imeinuka mpaka mawinguni.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 Tulijaribu kuuponya Babuloni, lakini hauwezi kuponywa. Uacheni, twendeni zetu, kila mmoja katika nchi yake, maana hukumu yake ni kuu mno imeinuka mpaka mawinguni.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 Tulijaribu kuuponya Babuloni, lakini hauwezi kuponywa. Uacheni, twendeni zetu, kila mmoja katika nchi yake, maana hukumu yake ni kuu mno imeinuka mpaka mawinguni.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 “ ‘Tungemponya Babeli, lakini hawezi kuponyeka; tumwacheni, na kila mmoja wetu aende nchi yake mwenyewe, kwa kuwa hukumu yake inafika angani, inapanda juu hadi mawinguni.’

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 “ ‘Tungemponya Babeli, lakini hawezi kuponyeka; tumwacheni, na kila mmoja wetu aende nchi yake mwenyewe, kwa kuwa hukumu yake inafika angani, inapanda juu hadi mawinguni.’

Tazama sura Nakili

Yeremia 51:9
13 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini kulikuwako huko nabii wa BWANA, jina lake aliitwa Odedi; akatoka kuwalaki jeshi waliokuja Samaria, akawaambia, Angalieni, kwa kuwa BWANA, Mungu wa baba zenu, aliwakasirikia Yuda, yeye amewatia mikononi mwenu, nanyi mmewaua kwa ghadhabu iliyofikia mbinguni.

nikasema, Ee Mungu wangu, nimetahayari, naona haya kuinua uso wangu mbele zako, Mungu wangu; kwa maana maovu yetu ni mengi, hata yamefika juu ya vichwa vyetu, na hatia yetu imeongezeka na kufika mbinguni.

Basi, itakuwa kama vile paa aliyetishwa, na kama kondoo wasio na mtu wa kuwakusanya; kila mtu atageukia watu wake; nao watakimbia, kila mtu aende nchi yake mwenyewe.

Ndivyo yatakavyokuwa mambo hayo uliyojitaabisha nayo; wale waliofanya biashara nawe tangu ujana wako watatangatanga mbali nawe, kila mtu akienda zake; hapatakuwa na mtu wa kukuokoa.

Aliwakwaza wengi, naam, wakaangukiana wao kwa wao; wakasema, Haya! Na tuondoke, tukarudi kwa watu wetu wenyewe, hadi nchi tuliyozaliwa, tuukimbie upanga unaotuonea.

Na askari wake waliojiwa, walio kati yake, Ni kama ndama walionona malishoni; Maana wao nao wamerudi nyuma, Wamekimbia wote pamoja, wasisimame; Maana siku ya msiba wao imewafikia, Wakati wa kujiliwa kwao.

Mpanzi mkatilie mbali na Babeli, Naye ashikaye mundu wakati wa mavuno; Kwa sababu ya kuuogopa upanga uoneao, Watageuka kila mtu kwa watu wake, Nao wataikimbilia kila mmoja nchi yake.

Mavuno yamepita, wakati wa joto umekwisha, wala sisi hatukuokoka.

Ole wao! Kwa kuwa wamenikimbia; uharibifu na uwapate! Kwa kuwa wameniasi; ingawa ninataka kuwakomboa, hata hivyo wamenena uongo juu yangu.

Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.

Kwa maana dhambi zake zimefika hata mbinguni, na Mungu amekumbuka maovu yake.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo