Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 51:57 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

57 Nami nitawalevya wakuu wake, na watu wake wenye hekima, watawala wake, na makamanda wake, na mashujaa wake; nao watalala usingizi wa milele, wasiamke, asema Mfalme, BWANA wa majeshi, ambaye jina lake ni BWANA.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

57 Nitawalewesha wakuu na wenye hekima wake, watawala wake, madiwani na askari wake; watalala usingizi wa milele wasiinuke tena. Nasema mimi mfalme ambaye jina langu ni Mwenyezi-Mungu wa Majeshi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

57 Nitawalewesha wakuu na wenye hekima wake, watawala wake, madiwani na askari wake; watalala usingizi wa milele wasiinuke tena. Nasema mimi mfalme ambaye jina langu ni Mwenyezi-Mungu wa Majeshi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

57 Nitawalewesha wakuu na wenye hekima wake, watawala wake, madiwani na askari wake; watalala usingizi wa milele wasiinuke tena. Nasema mimi mfalme ambaye jina langu ni Mwenyezi-Mungu wa Majeshi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

57 Nitawafanya maafisa wake na wenye busara walewe, watawala wao, maafisa, pamoja na mashujaa wao; watalala milele na hawataamka,” asema Mfalme, ambaye jina lake ni Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

57 Nitawafanya maafisa wake na wenye busara walewe, watawala wao, maafisa, pamoja na wapiganaji wao; watalala milele na hawataamka,” asema Mfalme, ambaye jina lake ni bwana Mwenye Nguvu Zote.

Tazama sura Nakili




Yeremia 51:57
20 Marejeleo ya Msalaba  

Basi malaika wa BWANA alitoka, akaua watu elfu mia moja na themanini na tano katika kituo cha Waashuri, na watu walipoamka asubuhi na mapema, kumbe, hao walikuwa maiti wote pia.


Nizitanguaye ishara za waongo, na kuwatia waganga wazimu; niwarudishaye nyuma wenye hekima, na kuyageuza maarifa yao kuwa ujinga;


Ndipo niliposema, Ole wangu! Kwa maana nimepotea; kwa sababu mimi ni mtu mwenye midomo michafu, nami ninakaa kati ya watu wenye midomo michafu; na macho yangu yamemwona Mfalme, BWANA wa majeshi.


Ndipo utakapowaambia, BWANA asema hivi, Tazama, nitawajaza ulevi wenyeji wote wa nchi hii, hata wafalme wanaoketi katika kiti cha enzi cha Daudi, na makuhani, na manabii, na wenyeji wote wa Yerusalemu.


Nawe utawaambia hivi, BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Nyweni, na kulewa, na kutapika, na kuanguka msiinuke tena, kwa sababu ya upanga nitakaoutuma kati yenu.


Kama mimi niishivyo, asema Mfalme, ambaye jina lake ni BWANA wa majeshi, hakika yake, kama Tabori katika milima, na kama Karmeli karibu na bahari, ndivyo atakavyokuja.


Moabu ameharibika, na moshi wa miji yake umepanda; na vijana wake wateule wameteremka kwenda kuchinjwa, asema Mfalme, ambaye jina lake ni BWANA wa majeshi.


Kwa sababu hiyo vijana wake wataanguka katika njia zake kuu, na watu wake wa vita, wote pia, watanyamazishwa katika siku hiyo, asema BWANA.


Wakiingiwa na ukali, nitawafanyia karamu yao, nami nitawalevya, wapate kufurahi, na kulala usingizi wa milele, wasiamke tena, asema BWANA.


Kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, hakika kwa mkono hodari, na kwa mkono ulionyoshwa, na kwa ghadhabu iliyomwagika, nitakuwa mfalme juu yenu;


Kwa maana kama miiba wametatana, kama walevi wamelewa, watateketezwa kama mabua makavu.


Wachungaji wako wanalala usingizi, Ee mfalme wa Ashuru; watu wako wenye heshima wamepumzika; watu wako wametawanyika juu ya milima, wala hapana mtu wa kuwakusanya.


Lakini na alaaniwe mtu adanganyaye, ambaye katika kundi lake ana dume, akaweka nadhiri, ila amtolea Bwana kitu kilicho na kilema; kwa maana mimi ni Mfalme mkuu, asema BWANA wa majeshi, na jina langu latisha katika mataifa.


Na hao wafalme wa nchi, waliozini naye na kufanya anasa pamoja naye, watalia na kumwombolezea; wauonapo moshi wa kuungua kwake;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo