Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yeremia 51:51 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

51 Twaona haya kwa kuwa tumesikia shutuma; Fedheha imetufunika nyuso zetu; Kwa sababu wageni wamepaingia Patakatifu pa nyumba ya BWANA.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

51 Mnasema: ‘Tumeaibishwa na kufadhaishwa; aibu imezifunika nyuso zetu, kwa sababu wageni wameingia katika sehemu takatifu za nyumba ya Mwenyezi-Mungu.’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

51 Mnasema: ‘Tumeaibishwa na kufadhaishwa; aibu imezifunika nyuso zetu, kwa sababu wageni wameingia katika sehemu takatifu za nyumba ya Mwenyezi-Mungu.’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

51 Mnasema: ‘Tumeaibishwa na kufadhaishwa; aibu imezifunika nyuso zetu, kwa sababu wageni wameingia katika sehemu takatifu za nyumba ya Mwenyezi-Mungu.’

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

51 “Tumetahayari, kwa sababu tumetukanwa na aibu imefunika nyuso zetu, kwa sababu wageni wameingia mahali patakatifu pa nyumba ya Mwenyezi Mungu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

51 “Tumetahayari, kwa maana tumetukanwa na aibu imefunika nyuso zetu, kwa sababu wageni wameingia mahali patakatifu pa nyumba ya bwana.”

Tazama sura Nakili




Yeremia 51:51
37 Marejeleo ya Msalaba  

Washitaki wangu watavikwa fedheha, Na wavikwe aibu yao kama joho.


Waaibishwe, watoweshwe, adui za nafsi yangu. Wavikwe laumu na aibu wanaonitakia mabaya.


Ee Mungu, mataifa wameingia katika urithi wako, Wamelinajisi hekalu lako takatifu. Wamefanya Yerusalemu chungu chungu.


Uwalipe jirani zetu mara saba vifuani mwao Laumu zao walizokulaumu, Ee Bwana.


Tumekuwa lawama kwa jirani zetu, Mzaha na dhihaka kwao wanaotuzunguka.


Hadi lini, Ee BWANA? Utajificha hata milele? Ghadhabu yako itawaka kama moto hadi lini?


Ufunuo juu ya Babeli; maono aliyoyaona Isaya, mwana wa Amozi.


Maana BWANA atamhurumia Yakobo, atamchagua Israeli tena, naye atawaweka katika nchi yao wenyewe; na mgeni atajiunga nao, nao wataambatana na nyumba ya Yakobo.


Ufunuo juu ya nyika kando ya bahari. Kama tufani za Negebu zikaribiavyo kwa kasi, inakuja kutoka kwa nyika, toka nchi itishayo.


Haya, shuka, keti mavumbini, Ewe bikira, binti Babeli; Keti chini pasipo kiti cha enzi, Ewe binti wa Wakaldayo; Maana hutaitwa tena mwororo, mpenda anasa.


Na wakuu wao huwatuma watoto wao kwenye maji; Nao hufika visimani wasipate maji; Hurudi, na vyombo vyao ni vitupu; Wametahayarika na kufadhaika, Na kuvifunika vichwa vyao.


na wafalme wote wa kaskazini, walio mbali na walio karibu, wote pamoja; na falme zote za dunia, zilizoko katika dunia; na mfalme wa Sheshaki atakunywa baada yao.


Hakika baada ya kukugeukia kwangu, nilitubu; na baada ya kufundishwa kwangu, nilijipiga pajani; nilitahayarika, naam, nilifadhaika, kwa sababu niliichukua aibu ya ujana wangu.


Akaiteketeza nyumba ya BWANA, na nyumba ya mfalme; na nyumba zote za Yerusalemu, naam, kila nyumba kubwa aliiteketeza kwa moto.


Huyo mtesi amenyosha mkono wake Juu ya matamanio yake yote; Maana ameona ya kuwa mataifa wameingia Ndani ya patakatifu pake; Ambao kwa habari zao wewe uliamuru Wasiingie katika kusanyiko lako.


Tazama, BWANA, uangalie, Ni nani uliyemtenda hayo! Je! Wanawake wale mazao yao, Watoto waliowabeba? Je! Kuhani na nabii wauawe Katika patakatifu pa Bwana?


Ee BWANA, kumbuka yaliyotupata; Utazame na kuiona aibu yetu.


Uwaambie nyumba ya Israeli, Bwana MUNGU asema hivi; Angalieni, nitapatia unajisi patakatifu pangu, fahari ya uwezo wenu, mahali pa kutamaniwa na macho yenu, ambapo roho zenu zinapahurumia na wana wenu na binti zenu, mliowaacha nyuma, wataanguka kwa upanga.


Nami nitazidisha matunda ya miti, na mazao ya mashamba, msipate tena kutukanwa na mataifa kwa sababu ya njaa.


Tena watajifungia nguo za magunia, na utisho utawafunika; na aibu itakuwa juu ya nyuso zote, na upaa juu ya vichwa vyao vyote.


Akawaambia, itieni nyumba unajisi, mkazijaze nyua mizoga ya hao waliouawa; haya, nendeni. Wakaenenda, wakaua watu katika mji.


Na wenye silaha watasimama upande wake, nao watapatia unajisi mahali patakatifu, ndiyo ngome, nao wataondoa sadaka ya kuteketezwa ya kila siku, nao watalisimamisha chukizo la uharibifu.


na mahali palipoinuka pa Isaka patakuwa ukiwa, na mahali patakatifu pa Israeli pataharibika; nami nitaondoka nishindane na nyumba ya Yeroboamu kwa upanga.


Kwa maana amri za Omri ndizo zishikwazo, na matendo yote ya nyumba ya Ahabu, nanyi mnakwenda katika mashauri yao; ili nikufanye kuwa ukiwa, na wenyeji waliomo humo kuwa zomeo; nanyi mtayachukua matukano waliyotukanwa watu wangu.


Ndipo adui yangu ataliona jambo hilo, na aibu itamfunika, yeye aliyeniambia, Yuko wapi BWANA, Mungu wako? Macho yangu yatamtazama; sasa atakanyagwa kama matope ya njia kuu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo