Yeremia 51:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC5 Kwa maana Israeli, wala Yuda, hakuachwa na Mungu wake, BWANA wa majeshi; ijapokuwa nchi yao imejaa hatia juu yake aliye Mtakatifu wa Israeli. Tazama suraMatoleo zaidiBiblia Habari Njema5 Lakini Israeli na Yuda hawakuachwa na Mungu wao Mwenyezi-Mungu wa majeshi, ingawa nchi yao imejaa hatia mbele yake yeye Mtakatifu wa Israeli. Tazama suraBiblia Habari Njema - BHND5 Lakini Israeli na Yuda hawakuachwa na Mungu wao Mwenyezi-Mungu wa majeshi, ingawa nchi yao imejaa hatia mbele yake yeye Mtakatifu wa Israeli. Tazama suraBiblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza5 Lakini Israeli na Yuda hawakuachwa na Mungu wao Mwenyezi-Mungu wa majeshi, ingawa nchi yao imejaa hatia mbele yake yeye Mtakatifu wa Israeli. Tazama suraNeno: Bibilia Takatifu5 Kwa maana Israeli na Yuda hawajaachwa na Mungu wao, Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, ingawa nchi yao imejaa uovu mbele zake yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli. Tazama suraNeno: Maandiko Matakatifu5 Kwa maana Israeli na Yuda hawajaachwa na Mungu wao, bwana Mwenye Nguvu Zote, ingawa nchi yao imejaa uovu mbele zake yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli. Tazama sura |
Siku hiyo nitawafanya wakuu wa Yuda kuwa kama kigae chenye moto katika kuni, na kama kinga cha moto katika miganda; nao watateketeza watu wa kila kabila, wawazungukao pande zote, upande wa mkono wa kulia na upande wa mkono wa kushoto; na baada ya haya Yerusalemu utakaa mahali pake, naam, hapo Yerusalemu.