Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 51:45 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

45 Enyi watu wangu; tokeni katikati yake, mkajiokoe nafsi zenu kutoka kwa hasira kali ya BWANA, kila mmoja wenu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

45 “Tokeni humo enyi watu wangu! Kila mtu na ayasalimishe maisha yake, kutoka hasira kali ya Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

45 “Tokeni humo enyi watu wangu! Kila mtu na ayasalimishe maisha yake, kutoka hasira kali ya Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

45 “Tokeni humo enyi watu wangu! Kila mtu na ayasalimishe maisha yake, kutoka hasira kali ya Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

45 “Tokeni ndani yake, enyi watu wangu! Okoeni maisha yenu! Ikimbieni hasira kali ya Mwenyezi Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

45 “Tokeni ndani yake, enyi watu wangu! Okoeni maisha yenu! Ikimbieni hasira kali ya bwana.

Tazama sura Nakili




Yeremia 51:45
13 Marejeleo ya Msalaba  

Haya, tokeni katika Babeli, Kimbieni kutoka kwa Wakaldayo; Hubirini kwa sauti ya kuimba, tangazeni haya, Yatamkeni mpaka mwisho wa dunia, semeni, BWANA amemkomboa mtumishi wake, Yakobo.


Sauti yao wakimbiao na kuokoka, Kutoka katika nchi ya Babeli, Ili kutangaza katika Sayuni kisasi cha BWANA, Mungu wetu, Kisasi cha hekalu lake.


Kimbieni kutoka kati ya Babeli, mkatoke katika nchi ya Wakaldayo, mkawe kama mabeberu mbele ya makundi.


Ninyi mliojiepusha na upanga, Nendeni zenu, msisimame; Mkumbukeni BWANA tokea mbali, Na Yerusalemu ukatiwe mioyoni mwenu.


Kimbieni kutoka kati ya Babeli, kila mtu na ajiokoe nafsi yake; msikatiliwe mbali katika uovu wake; maana ni wakati wa kisasi cha BWANA, atamlipa malipo.


Tungependa kuuponya Babeli, Lakini haukuponyeka; Mwacheni, nasi twendeni zetu, Kila mtu hata nchi yake mwenyewe; Maana hukumu yake inafika hata mbinguni, Nayo imeinuliwa kufikia mawinguni.


Haya! Ee Sayuni, jiponye, wewe ukaaye pamoja na binti Babeli.


Akasema na mkutano, na kuwaambia, Nawasihi, ondokeni penye hema za hawa watu waovu, wala msiguse kitu chao chochote, msiangamizwe katika dhambi zao zote.


Akawashuhudia kwa maneno mengine mengi sana na kuwaonya, akisema, Jiokoeni na kizazi hiki chenye ukaidi.


Kwa hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema Bwana, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha.


Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo