Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 51:36 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

36 Basi, BWANA asema hivi, Tazama, nitakutetea, nami nitatwaa kisasi kwa ajili yako; nami nitaikausha bahari yake, nitaifanya chemchemi yake kuwa pakavu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

36 Kwa hiyo asema hivi Mwenyezi-Mungu: “Nitawatetea kuhusu kisa chenu, na kulipiza kisasi kwa ajili yenu. Nitaikausha bahari ya Babuloni na kuvifanya visima vyake vikauke.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

36 Kwa hiyo asema hivi Mwenyezi-Mungu: “Nitawatetea kuhusu kisa chenu, na kulipiza kisasi kwa ajili yenu. Nitaikausha bahari ya Babuloni na kuvifanya visima vyake vikauke.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

36 Kwa hiyo asema hivi Mwenyezi-Mungu: “Nitawatetea kuhusu kisa chenu, na kulipiza kisasi kwa ajili yenu. Nitaikausha bahari ya Babuloni na kuvifanya visima vyake vikauke.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

36 Kwa hiyo, hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: “Tazama, nitakutetea na kukulipizia kisasi; nitaikausha bahari yake na kuzikausha chemchemi zake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

36 Kwa hiyo, hili ndilo bwana asemalo: “Tazama, nitatetea shauri lako na kulipiza kisasi kwa ajili yako; nitaikausha bahari yake na kuzikausha chemchemi zake.

Tazama sura Nakili




Yeremia 51:36
24 Marejeleo ya Msalaba  

Amegeuza mito ikawa jangwa, Na chemchemi za maji zikawa nchi kavu.


Najua ya kuwa BWANA atamfanyia mnyonge hukumu, Na wahitaji haki yao.


Kwa sababu BWANA atawatetea; Naye atawateka uhai wao waliowateka.


Kwa sababu mkombozi wao ana nguvu; Atawatetea juu yako.


Na maji ya baharini yatapunguka, na huo mto utakauka na kuwa pakavu.


BWANA, Mkombozi wenu, Mtakatifu wa Israeli, asema hivi; Kwa ajili yenu nimetuma ujumbe Babeli nami nitawashusha wote mfano wa wakimbizi, naam, Wakaldayo, katika merikebu zao walizozifurahia.


niviambiaye vilindi, Kauka, nami nitaikausha mito yako;


Ukosefu wa mvua uko juu ya maji yake, nayo yatakaushwa; maana ni nchi ya sanamu za kuchongwa, nao wameingiwa na wazimu kwa ajili ya sanamu.


Inoeni hiyo mishale; zishikeni ngao kwa nguvu; BWANA ameziamsha roho za wafalme wa Wamedi; kwa sababu shauri lake ni juu ya Babeli auangamize; maana ni kisasi cha BWANA, kisasi cha hekalu lake.


Kimbieni kutoka kati ya Babeli, kila mtu na ajiokoe nafsi yake; msikatiliwe mbali katika uovu wake; maana ni wakati wa kisasi cha BWANA, atamlipa malipo.


Nami nitaweka kisasi changu juu ya Edomu, kwa mkono wa watu wangu Israeli; nao watatenda mambo katika Edomu, kwa kadiri ya hasira yangu, na ghadhabu yangu, nao watakijua kisasi changu, asema Bwana MUNGU.


Ajapokuwa yeye ni mwenye kuzaa sana kati ya ndugu zake, upepo wa mashariki utakuja, hiyo pumzi ya BWANA itokayo upande wa nyikani, na kijito chake cha maji kitakauka, na chemchemi yake itakaushwa; yeye atateka nyara hazina ya vyombo vyote vipendezavyo.


Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana.


Kisasi ni changu mimi, na kulipa, Wakati itakapoteleza miguu yao; Maana siku ya msiba wao imekaribia, Na mambo yatakayowapata yatafanya haraka.


Furahini, enyi mataifa, pamoja na watu wake; Kwa maana atatwaa kisasi kwa damu ya watumwa wake, Atawatoza kisasi adui zake, Tena atafanya kafara kwa nchi yake, na watu wake.


Na huyo wa sita akalimimina bakuli lake juu ya mto ule mkubwa Frati; maji yake yakakauka, ili njia itengenezwe kwa wafalme watokao katika maawio ya jua.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo