Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 51:29 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

29 Nayo nchi yatetemeka, nayo ina uchungu; maana makusudi ya BWANA juu ya Babeli yasimama, kuifanya nchi ya Babeli ukiwa, isikaliwe na mtu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

29 Nchi inatetemeka na kugaagaa kwa maumivu, maana nia ya Mwenyezi-Mungu kuhusu Babuloni ni thabiti: Ataifanya nchi ya Babuloni kuwa jangwa, ataifanya iwe bila watu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

29 Nchi inatetemeka na kugaagaa kwa maumivu, maana nia ya Mwenyezi-Mungu kuhusu Babuloni ni thabiti: Ataifanya nchi ya Babuloni kuwa jangwa, ataifanya iwe bila watu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

29 Nchi inatetemeka na kugaagaa kwa maumivu, maana nia ya Mwenyezi-Mungu kuhusu Babuloni ni thabiti: ataifanya nchi ya Babuloni kuwa jangwa, ataifanya iwe bila watu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

29 Nchi inatetemeka na kugaagaa, kwa kuwa makusudi ya Mwenyezi Mungu dhidi ya Babeli yanasimama: yaani kuangamiza nchi ya Babeli ili pasiwepo atakayeishi humo.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

29 Nchi inatetemeka na kugaagaa, kwa kuwa makusudi ya bwana dhidi ya Babeli yanasimama: yaani, kuangamiza nchi ya Babeli ili pasiwe na yeyote atakayeishi humo.

Tazama sura Nakili




Yeremia 51:29
25 Marejeleo ya Msalaba  

Wao wakuonao watakukazia macho, Watakuangalia sana, wakisema, Je! Huyu ndiye aliyeitetemesha dunia, Huyu ndiye aliyetikisa falme;


Dunia inalewalewa kama mlevi, nayo inawayawaya kama machela; na mzigo wa dhambi zake utailemea; nayo itaanguka, wala haitainuka tena.


Bali BWANA ndiye Mungu wa kweli; Ndiye Mungu aliye hai, Mfalme wa milele; Mbele za ghadhabu yake nchi yatetemeka, Wala mataifa hawawezi kustahimili hasira yake.


Kwa sababu ya ghadhabu ya BWANA haitakaliwa na mtu, bali itakuwa ukiwa mtupu; kila mtu apitaye karibu na Babeli atashangaa, atazomea kwa sababu ya mapigo yake yote.


Upanga uko juu ya hao wajisifuo, nao watapumbazika; upanga uko juu ya mashujaa wake, nao watafadhaika.


Mfalme wa Babeli amesikia habari zao, Na mikono yake imekuwa dhaifu; Dhiki imemshika, na maumivu, Kama ya mwanamke akiwa katika uchungu wa kujifungua.


Basi, lisikieni shauri la BWANA, Alilolifanya juu ya Babeli; Na makusudi yake aliyoyakusudia Juu ya nchi ya Wakaldayo. Hakika watawaburura, naam, wadogo wa kundi; Hakika malisho yao yatafadhaika kwa ajili yao.


Kwa kishindo cha kutwaliwa Babeli nchi itatetemeka, Na kilio chake chasikiwa katika mataifa.


Wala hawatatwaa kwako jiwe moja liwe la pembeni, wala jiwe moja liwe msingi; bali wewe utakuwa ukiwa daima, asema BWANA.


Wekeni mataifa tayari juu yake, wafalme wa Wamedi, na watawala wake, na wakuu wake, na nchi yote ya mamlaka yake.


Na Babeli utakuwa magofu, makao ya mbwamwitu, ajabu, na mazomeo, pasipo mtu wa kukaa huko.


Miji yake imekuwa maganjo; Nchi ya ukame, na jangwa; Nchi asimokaa mtu yeyote, Wala hapiti mwanadamu huko.


Kutoka Dani kumesikiwa mkoromo wa farasi wake; nchi yote pia inatetemeka kwa sauti ya mlio wa farasi wake wa vita; maana wamekuja, wamekula nchi na vyote vilivyomo; huo mji na wote wakaao ndani yake.


Nchi inatetemeka mbele yao; mbingu zinatetemeka; jua na mwezi hutiwa giza, na nyota huacha kuangaza;


Kwa ajili ya hayo, je! Haitatetemeka nchi, na kuomboleza kila mtu akaaye ndani yake? Naam, itainuka yote pia kama huo Mto; nayo itataabika na kupwa tena kama Mto wa Misri.


Akalia kwa sauti kuu, akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli ulio mkuu; umekuwa maskani ya mashetani, na ngome ya kila roho mchafu, na ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo