Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 51:27 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

27 Itwekeni bendera katika nchi, pigeni tarumbeta kati ya mataifa, yawekeni mataifa tayari juu yake; ziiteni juu yake falme za Ararati, na Mini, na Ashkenazi; agizeni jemadari juu yake; wapandisheni farasi, kama tunutu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

27 Tweka bendera ya vita duniani, piga tarumbeta kati ya mataifa; yatayarishe mataifa kupigana naye; ziite falme kuishambulia; falme za Ararati, Mini na Ashkenazi. Weka majemadari dhidi yake; walete farasi kama makundi ya nzige.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

27 Tweka bendera ya vita duniani, piga tarumbeta kati ya mataifa; yatayarishe mataifa kupigana naye; ziite falme kuishambulia; falme za Ararati, Mini na Ashkenazi. Weka majemadari dhidi yake; walete farasi kama makundi ya nzige.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

27 Tweka bendera ya vita duniani, piga tarumbeta kati ya mataifa; yatayarishe mataifa kupigana naye; ziite falme kuishambulia; falme za Ararati, Mini na Ashkenazi. Weka majemadari dhidi yake; walete farasi kama makundi ya nzige.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

27 “Inueni bendera katika nchi! Pigeni tarumbeta katikati ya mataifa! Andaeni mataifa kwa ajili ya vita dhidi yake, iteni falme hizi dhidi yake: Ararati, Mini na Ashkenazi. Wekeni jemadari dhidi yake, pelekeni farasi wengi kama kundi la nzige.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

27 “Twekeni bendera katika nchi! Pigeni tarumbeta katikati ya mataifa! Andaeni mataifa kwa ajili ya vita dhidi yake, iteni falme hizi dhidi yake: Ararati, Mini na Ashkenazi. Wekeni jemadari dhidi yake, pelekeni farasi wengi kama kundi la nzige.

Tazama sura Nakili




Yeremia 51:27
24 Marejeleo ya Msalaba  

Na wana wa Gomeri ni Ashkenazi, na Rifathi, na Togama.


Mwezi wa saba, siku ya kumi na saba ya mwezi, safina ikatua juu ya milima ya Ararati.


Ikawa, alipokuwa akiabudu nyumbani mwa Nisroki, mungu wake, Adrameleki na Shareza wakampiga kwa upanga; wakaikimbilia nchi ya Ararati. Na Esar-hadoni mwanawe akatawala mahali pake.


Na wana wa Gomeri; Ashkenazi, na Rifathi, na Togama.


Enyi watu mkaao katika ulimwengu wote, na wenyeji wa dunia, bendera ikiinuliwa milimani, angalieni; na wakipiga tarumbeta, sikieni.


Ikawa alipokuwa akiabudu katika nyumba ya Nisroki, mungu wake, Adrameleki na Shareza, wanawe, wakampiga kwa upanga; wakakimbilia nchi ya Ararati; naye Esar-hadoni, mwanawe, akatawala baada yake.


Kwa maana mataifa mengi na wafalme wakuu watawatumikisha; naam, hao pia; nami nitawalipa kwa kadiri ya matendo yao, na kwa kadiri ya kazi ya mikono yao.


Wataukata msitu wake, asema BWANA, ingawa haupenyeki; Kwa maana ni wengi kuliko nzige, hawahesabiki.


Tangazeni katika mataifa, Mkahubiri na kutweka bendera; Hubirini, msifiche, semeni, Babeli umetwaliwa! Beli amefedheheka; Merodaki amefadhaika; Sanamu zake zimeaibishwa, Vinyago vyake vimefadhaika.


Maana toka kaskazini taifa linakuja juu yake, litakaloifanya nchi yake kuwa ukiwa; wala hakuna mtu atakayekaa humo; wamekimbia, wamekwenda zao, mwanadamu na mnyama pia.


Kwa maana juu ya Babeli nitaamsha na kuleta kusanyiko la mataifa makubwa, toka nchi ya kaskazini; nao watajipanga juu yake; kutoka huko atatwaliwa; mishale yao itakuwa kama ya mtu shujaa aliye stadi; hakuna hata mmoja utakaorudi bure.


Twekeni bendera ya vita juu ya kuta za Babeli, imarisheni ulinzi, wawekeni walinzi, tayarisheni waviziao; kwa maana BWANA ameazimia na kutenda yote aliyoyasema juu yao wakaao Babeli.


BWANA wa majeshi ameapa kwa nafsi yake, akisema, Hakika nitakujaza watu, kama nzige, nao watapiga kelele juu yako.


Wekeni mataifa tayari juu yake, wafalme wa Wamedi, na watawala wake, na wakuu wake, na nchi yote ya mamlaka yake.


Kimbieni mpate kuwa salama, enyi wana wa Benyamini; tokeni katika Yerusalemu, pigeni tarumbeta katika Tekoa, simamisheni ishara juu ya Beth-hakeremu; kwa maana mabaya yanachungulia toka kaskazini, na uharibifu mkuu.


Tangazeni haya kati ya mataifa; jitayarisheni kwa vita; waamsheni mashujaa; watu wa vita na wakaribie; na wapande juu.


Je! Tarumbeta itapigwa mjini, watu wasiogope? Mji utapatikana na hali mbaya, asiyoileta BWANA?


Kwa maana nitawakusanya mataifa yote walete vita juu ya Yerusalemu; na huo mji utapigwa, nazo nyumba zitatekwa, nao wanawake watatendwa jeuri; na nusu ya watu wa mji watatoka kwenda utumwani; ila mabaki ya watu wa mji hawatakatiliwa mbali.


Kwa maana walikwea na ng'ombe zao na hema zao, wakaja mfano wa nzige kwa wingi; wao na ngamia zao pia walikuwa hawana hesabu; nao waliingia katika hiyo nchi ili kuiharibu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo