Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yeremia 51:21 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

21 na kwa wewe nitamvunjavunja farasi, na yeye ampandaye; na kwa wewe nitalivunjavunja gari la vita, na yeye achukuliwaye ndani yake;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

21 Nakutumia kuponda farasi na wapandafarasi, magari ya kukokotwa na waendeshaji wake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

21 Nakutumia kuponda farasi na wapandafarasi, magari ya kukokotwa na waendeshaji wake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

21 Nakutumia kuponda farasi na wapandafarasi, magari ya kukokotwa na waendeshaji wake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

21 kwa wewe navunjavunja farasi na mpanda farasi, kwa wewe navunjavunja gari la vita na mwendeshaji wake,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

21 kwa wewe navunjavunja farasi na mpanda farasi, kwa wewe navunjavunja gari la vita na mwendeshaji wake,

Tazama sura Nakili




Yeremia 51:21
14 Marejeleo ya Msalaba  

Avikomesha vita hata mwisho wa dunia; Avunja uta, akata mkuki, achoma moto magari.


Kwa kukemea kwako, Ee Mungu wa Yakobo, Gari na farasi wameshikwa na usingizi mzito.


Ndipo Musa na wana wa Israeli wakamwimbia BWANA wimbo huu wakanena, na kusema, Nitamwimbia BWANA, kwa maana ametukuka sana; Farasi na mpanda farasi amewatupa baharini.


Miriamu akawaitikia, Mwimbieni BWANA kwa maana ametukuka sana; Farasi na mpanda farasi amewatupa baharini.


Magari ya Farao na jeshi lake amewatupa baharini, Maofisa wake wateule wamezama katika Bahari ya Shamu.


atoaye gari na farasi, jeshi la askari na uwezo; wamelala, hawataondoka; wametoweka, wamezimwa kama utambi.


Upanga uko juu ya farasi wao, na juu ya magari yao ya vita; na juu ya watu wote waliochanganyika ndani yake, nao watakuwa kama wanawake; upanga u juu ya hazina zake, nazo zitaibwa.


Nanyi mtashibishwa mezani pangu kwa farasi, na magari ya vita, na mashujaa, na watu wote wa vita, asema Bwana MUNGU.


Kisha itakuwa katika siku hiyo, asema BWANA, nitawakatilia mbali farasi wako watoke kati yako, nami nitayaharibu magari yako ya vita;


Tazama, mimi ni juu yako, asema BWANA wa majeshi, nami nitayateketeza magari yako ya vita katika moshi, na upanga utawaangamiza wanasimba wako; nami nitayakatilia mbali mawindo yako katika nchi, na sauti za wajumbe wako hazitasikiwa tena kamwe.


nami nitakipindua kiti cha enzi cha falme, nami nitaziharibu nguvu za falme za mataifa; nami nitayapindua magari, na hao wapandao ndani yake; farasi na hao wawapandao wataanguka chini; kila mtu kwa upanga wa ndugu yake.


Nao watakuwa kama mashujaa, wakanyagao adui zao katika matope ya njia vitani; nao watapiga vita, kwa sababu BWANA yu pamoja nao; na hao wapandao farasi watafadhaishwa.


Katika siku hiyo, asema BWANA, nitamtia kila farasi ushangao, na yeye ampandaye nitamtia wazimu; nami nitaifunulia nyumba ya Yuda macho yangu, nami nitamtia upofu kila farasi wa hayo makabila ya watu.


mpate kula nyama ya wafalme, na nyama ya majemadari, na nyama ya watu hodari, na nyama ya farasi na ya watu wawapandao, na nyama ya watu wote, waungwana kwa watumwa, wadogo kwa wakubwa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo