Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 51:19 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

19 Yeye, Fungu la Yakobo, siye kama hawa; Maana ndiye aliyeviumba vitu vyote; Na Israeli ni kabila la urithi wake; BWANA wa majeshi ndilo jina lake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

19 Mungu aliye hazina ya Yakobo si kama hizo, maana yeye ndiye aliyeviumba vitu vyote, na Israeli ni kabila lililo mali yake; Mwenyezi-Mungu wa Majeshi, ndilo jina lake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

19 Mungu aliye hazina ya Yakobo si kama hizo, maana yeye ndiye aliyeviumba vitu vyote, na Israeli ni kabila lililo mali yake; Mwenyezi-Mungu wa Majeshi, ndilo jina lake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

19 Mungu aliye hazina ya Yakobo si kama hizo, maana yeye ndiye aliyeviumba vitu vyote, na Israeli ni kabila lililo mali yake; Mwenyezi-Mungu wa Majeshi, ndilo jina lake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

19 Yeye Aliye Fungu la Yakobo sivyo alivyo, kwani ndiye Muumba wa vitu vyote, pamoja na kabila la urithi wake: Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni ndilo jina lake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

19 Yeye Aliye Fungu la Yakobo sivyo alivyo, kwani ndiye Muumba wa vitu vyote, pamoja na kabila la urithi wake: bwana Mwenye Nguvu Zote ndilo jina lake.

Tazama sura Nakili




Yeremia 51:19
19 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini Mungu wetu yuko mbinguni, Alitakalo lote amelitenda.


Kwa sababu BWANA amejichagulia Yakobo, Na Israeli, wawe watu wake hasa.


BWANA ndiye fungu la posho langu, Na la kikombe changu; Wewe unayaamua maisha yangu.


Heri taifa ambalo BWANA ni Mungu wao, Watu aliowachagua kuwa urithi wake.


Mwili wangu na moyo wangu hupunguka, Bali Mungu ni mwamba wa moyo wangu Na sehemu yangu milele.


Ulikumbuke kusanyiko lako, Ulilolinunua zamani. Ulilolikomboa liwe kabila la urithi wako, Mlima Sayuni ulioufanya maskani yako.


Mkombozi wetu, BWANA wa majeshi ndilo jina lake, Mtakatifu wa Israeli.


Ukamsahau BWANA, Muumba wako, yeye aliyezitanda mbingu, na kuiweka misingi ya dunia; nawe unaogopa daima mchana kutwa kwa sababu ya ghadhabu yake yeye aoneaye, hapo ajitayarishapo kuharibu; nayo i wapi ghadhabu yake aoneaye?


Ameiumba dunia kwa uweza wake, Ameuthibitisha ulimwengu kwa hekima yake, Na kwa ufahamu wake amezitandika mbingu.


Yeye, Fungu la Yakobo, siye kama hawa; Maana ndiye aliyeviumba vitu vyote; Na Israeli ni kabila la urithi wake; BWANA wa majeshi ndilo jina lake.


BWANA alitendaye jambo hili, BWANA aliumbaye ili alithibitishe; BWANA ndilo jina lake; asema hivi,


Kwa sababu mnafurahi, kwa sababu mnashangilia, enyi mnaouteka urithi wangu, kwa sababu mmenona kama mtamba akanyagaye nafaka, nanyi mnalia kama farasi wenye nguvu;


Mkombozi wao ni hodari; BWANA wa majeshi ndilo jina lake; yeye atawatetea kwa bidii, apate kuistarehesha nchi, na kuwasumbua wakaao katika Babeli.


Kwa maana Israeli, wala Yuda, hakuachwa na Mungu wake, BWANA wa majeshi; ijapokuwa nchi yao imejaa hatia juu yake aliye Mtakatifu wa Israeli.


BWANA ndiye fungu langu, husema nafsi yangu, Kwa hiyo nitamtumaini yeye.


Maana, sehemu ya BWANA ni watu wake, Yakobo ni kura ya urithi wake.


Bali ninyi ni uzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo