Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 51:14 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

14 BWANA wa majeshi ameapa kwa nafsi yake, akisema, Hakika nitakujaza watu, kama nzige, nao watapiga kelele juu yako.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Mwenyezi-Mungu wa majeshi ameapa kwa nafsi yake: “Hakika nitakujaza majeshi mengi kama nzige, nayo yatapiga vigelegele vya ushindi juu yako”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 Mwenyezi-Mungu wa majeshi ameapa kwa nafsi yake: “Hakika nitakujaza majeshi mengi kama nzige, nayo yatapiga vigelegele vya ushindi juu yako”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Mwenyezi-Mungu wa majeshi ameapa kwa nafsi yake: “Hakika nitakujaza majeshi mengi kama nzige, nayo yatapiga vigelegele vya ushindi juu yako”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni ameapa kwa nafsi yake mwenyewe: ‘Hakika nitakujaza na watu, kama kundi la nzige, nao watashangilia kwa ushindi juu yako.’

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 bwana Mwenye Nguvu Zote ameapa kwa nafsi yake mwenyewe: ‘Hakika nitakujaza na watu, kama kundi la nzige, nao watapiga kelele za ushindi juu yako.’

Tazama sura Nakili




Yeremia 51:14
13 Marejeleo ya Msalaba  

Alisema, kukaja nzige, Na tunutu wasiohesabika;


Basi, kwa sababu hiyo lisikieni neno la BWANA, ninyi nyote wa Yuda, mnaokaa katika nchi ya Misri, Tazama, nimeapa kwa jina langu kuu, asema BWANA, ya kwamba jina langu halitatajwa tena katika kinywa cha mtu awaye yote wa Yuda, katika nchi yote ya Misri, akisema, Kama Bwana MUNGU aishivyo!


Wataukata msitu wake, asema BWANA, ingawa haupenyeki; Kwa maana ni wengi kuliko nzige, hawahesabiki.


Kwa maana nimeapa kwa nafsi yangu, asema BWANA, kwamba Bozra utakuwa ajabu, na aibu, na ukiwa, na laana; na miji yake yote itakuwa ukiwa wa daima.


Mpigieni kelele pande zote; amejitoa; Maboma yake yameanguka, kuta zake zimebomolewa; Kwa maana ni kisasi cha BWANA; mlipizeni kisasi; Kama yeye alivyotenda, mtendeni yeye.


Itwekeni bendera katika nchi, pigeni tarumbeta kati ya mataifa, yawekeni mataifa tayari juu yake; ziiteni juu yake falme za Ararati, na Mini, na Ashkenazi; agizeni jemadari juu yake; wapandisheni farasi, kama tunutu.


Nami nitawarudishia hiyo miaka iliyoliwa na nzige, na parare, na madumadu, na tunutu, jeshi langu kubwa nililotuma kati yenu.


Bwana MUNGU ameapa kwa nafsi yake, asema BWANA, Mungu wa majeshi; Naizira fahari ya Yakobo, nachukizwa na majumba yake; kwa sababu hiyo nitautoa huo mji, pamoja na wote waliomo ndani yake.


Kwa maana Mungu, alipompa Abrahamu ahadi, kwa sababu alikuwa hana mkubwa kuliko yeye mwenyewe wa kumwapa, aliapa kwa nafsi yake,


Kwa maana walikwea na ng'ombe zao na hema zao, wakaja mfano wa nzige kwa wingi; wao na ngamia zao pia walikuwa hawana hesabu; nao waliingia katika hiyo nchi ili kuiharibu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo