Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 51:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

1 BWANA asema hivi, Angalia, nitaamsha juu ya Babeli, na juu yao wakaao Leb-kamai, upepo uharibuo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Nitachochea upepo wa kuangamiza dhidi ya Babuloni, dhidi ya wakazi wa Kaldayo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Nitachochea upepo wa kuangamiza dhidi ya Babuloni, dhidi ya wakazi wa Kaldayo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Nitachochea upepo wa kuangamiza dhidi ya Babuloni, dhidi ya wakazi wa Kaldayo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: “Tazama nitaamsha roho ya mwangamizi dhidi ya Babeli na wenyeji wa Leb-Kamai.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Hili ndilo asemalo bwana: “Tazama nitaamsha roho ya mwangamizi dhidi ya Babeli na watu wakaao Leb-Kamai.

Tazama sura Nakili




Yeremia 51:1
23 Marejeleo ya Msalaba  

Tazama, nitatia roho ya hofu ndani yake, naye atasikia uvumi, na kuirudia nchi yake mwenyewe; nami nitamwangusha kwa upanga katika nchi yake mwenyewe.


Ee binti Babeli, uliye karibu na kuangamia, Heri atakayekupatiliza, ulivyotupatiliza sisi.


Kwa hiyo nitazitetemesha mbingu, na dunia itatikiswa itoke katika mahali pake, kwa sababu ya ghadhabu ya BWANA wa majeshi, na kwa sababu ya siku ya hasira yake kali.


Nitapaa kupita vimo vya mawingu, Nitafanana na yeye Aliye Juu.


Ufunuo juu ya nyika kando ya bahari. Kama tufani za Negebu zikaribiavyo kwa kasi, inakuja kutoka kwa nyika, toka nchi itishayo.


Haya, shuka, keti mavumbini, Ewe bikira, binti Babeli; Keti chini pasipo kiti cha enzi, Ewe binti wa Wakaldayo; Maana hutaitwa tena mwororo, mpenda anasa.


Tazama, tufani ya BWANA, yaani, ghadhabu yake, imetokea; ni kimbunga cha tufani; itapasuka, na kuwaangukia waovu vichwani.


Na juu ya Elamu nitazileta pepo nne, toka pembe nne za mbinguni, nami nitawatawanya katika pande zote nne, wala hakuna taifa ambalo hawatalifikia watu wa Elamu waliofukuzwa.


Panda juu ya nchi ya Merathaimu, naam, juu yake, na juu yao wakaao Pekodi; ua, ukaangamize nyuma yao, asema BWANA, ukatende kama nilivyokuagiza, yote pia.


Nimekutegea mtego, Ee Babeli, nawe ukanaswa, nawe ulikuwa huna habari; umeonekana, ukakamatwa, kwa sababu ulishindana na BWANA.


Waiteni wapiga mishale juu ya Babeli, Naam, wote waupindao upinde; Pangeni hema kumzunguka pande zote; Ili asiokoke hata mtu mmoja wao; Mlipeni kwa kadiri ya kazi yake; Mtendeni sawasawa na yote aliyoyatenda; Kwa sababu amefanya kiburi juu ya BWANA, Juu yake aliye Mtakatifu wa Israeli.


BWANA wa majeshi asema hivi, Wana wa Israeli, na wana wa Yuda wameonewa sana, na pia wana wa Yuda vivyo hivyo, watekaji wao wote wamewashikilia sana; na wamekataa kuwaachilia waondoke.


Kwa maana juu ya Babeli nitaamsha na kuleta kusanyiko la mataifa makubwa, toka nchi ya kaskazini; nao watajipanga juu yake; kutoka huko atatwaliwa; mishale yao itakuwa kama ya mtu shujaa aliye stadi; hakuna hata mmoja utakaorudi bure.


Babeli ujapopanda mbinguni, na ujapopafanya mahali pa juu penye nguvu zake kuwa ngome, hata hivyo toka kwangu wenye kuangamiza watamwendea, asema BWANA.


Naye Yeremia akaandika katika kitabu kuhusu mabaya yote yatakayoupata Babeli, maneno hayo yote yaliyoandikwa juu ya Babeli.


Lakini aling'olewa kwa ghadhabu, akaangushwa chini, upepo wa mashariki ukakausha matunda yake; vijiti vyake vya nguvu vikavunjika, vikakauka; moto ulivila.


Ajapokuwa yeye ni mwenye kuzaa sana kati ya ndugu zake, upepo wa mashariki utakuja, hiyo pumzi ya BWANA itokayo upande wa nyikani, na kijito chake cha maji kitakauka, na chemchemi yake itakaushwa; yeye atateka nyara hazina ya vyombo vyote vipendezavyo.


Je! Tarumbeta itapigwa mjini, watu wasiogope? Mji utapatikana na hali mbaya, asiyoileta BWANA?


Kwa maana BWANA wa majeshi asema hivi, Ili nitafute utukufu amenituma kwa mataifa wale waliowateka ninyi; maana yeye awagusaye ninyi aigusa mboni ya jicho lake.


Akaanguka chini, akasikia sauti ikimwambia, Sauli, Sauli, mbona wanitesa?


Tufuate:

Matangazo


Matangazo