Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 50:46 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

46 Kwa kishindo cha kutwaliwa Babeli nchi itatetemeka, Na kilio chake chasikiwa katika mataifa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

46 Kwa kishindo cha kutekwa kwa Babuloni dunia itatetemeka, na kilio chake kitasikika miongoni mwa mataifa mengine.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

46 Kwa kishindo cha kutekwa kwa Babuloni dunia itatetemeka, na kilio chake kitasikika miongoni mwa mataifa mengine.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

46 Kwa kishindo cha kutekwa kwa Babuloni dunia itatetemeka, na kilio chake kitasikika miongoni mwa mataifa mengine.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

46 Kwa sauti ya kutekwa kwa Babeli, dunia itatetemeka; kilio chake kitasikika pote miongoni mwa mataifa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

46 Kwa sauti ya kutekwa kwa Babeli, dunia itatetemeka; kilio chake kitasikika pote miongoni mwa mataifa.

Tazama sura Nakili




Yeremia 50:46
14 Marejeleo ya Msalaba  

Moyo wangu unamlilia Moabu; wakuu wake wanakimbilia Soari kama ndama wa miaka mitatu; kwa maana wanapanda mbavu za Luhithi wakilia; maana katika njia iendayo hata Horonaimu wanatoa kilio cha maangamizi.


Kwa maana shamba la mizabibu la BWANA wa majeshi ndilo nyumba ya Israeli, na watu wa Yuda ni mche wake wa kupendeza; akatumaini kuona hukumu ya haki, na kumbe! Aliona dhuluma; alitumaini kuona haki, na kumbe! Alisikia kilio.


Bali BWANA ndiye Mungu wa kweli; Ndiye Mungu aliye hai, Mfalme wa milele; Mbele za ghadhabu yake nchi yatetemeka, Wala mataifa hawawezi kustahimili hasira yake.


Mataifa wamesikia habari za aibu yako, nayo dunia imejaa kilio chako; maana shujaa amejikwaa juu ya shujaa mwenzake, wameanguka wote wawili pamoja.


Angalia, atapanda kama simba toka kiburi cha Yordani juu ya malisho yasiyonyauka; lakini nitamkimbiza ghafla ayaache; na yeye aliye mteule nitamweka juu yake; maana ni nani aliye kama mimi? Tena ni nani atakayeniandikia muda? Tena ni mchungaji yupi atakayesimama mbele zangu?


Nchi yatetemeka kwa sauti ya kuanguka kwao; Kuna kilio, sauti yake yasikiwa katika Bahari ya Shamu.


Nayo nchi yatetemeka, nayo ina uchungu; maana makusudi ya BWANA juu ya Babeli yasimama, kuifanya nchi ya Babeli ukiwa, isikaliwe na mtu.


Sauti ya kilio kutoka Babeli, Na ya uangamizi mkuu toka nchi ya Wakaldayo!


Sasa visiwa vitatetemeka katika siku ya kuanguka kwako; naam, visiwa vilivyo katika bahari vitafadhaika, kwa sababu ya kuondoka kwako.


Kwa sauti ya vilio vya rubani zako viunga vyako vitatetemeka.


Niliwatetemesha mataifa kwa mshindo wa kuanguka kwake, hapo nilipomtupa chini mpaka kuzimu, pamoja nao washukao shimoni; na miti yote ya Adeni, miti iliyo miteule na iliyo mizuri ya Lebanoni, yote inywayo maji, ilifarijika pande za chini za nchi.


Nami nitawashangaza watu wa kabila nyingi kwa habari zako, na wafalme wao wataogopa sana kwa ajili yako, nitakapoutikisa upanga wangu mbele yao; nao watatetemeka kila dakika, kila mtu kwa ajili ya uhai wake, katika siku ya kuanguka kwako.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo