Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 50:42 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

42 Wanashika upinde na mkuki; Ni wakatili, hawana huruma; Sauti yao inanguruma kama bahari, Nao wamepanda farasi; Kila mmoja amejipanga kama aendaye vitani, Juu yako, Ee binti Babeli.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

42 Wameshika pinde zao na mikuki; ni watu wakatili na wasio na huruma. Vishindo vyao ni kama mvumo wa bahari, wamepanda farasi. Wamejipanga tayari kwa vita, dhidi yako wewe Babuloni!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

42 Wameshika pinde zao na mikuki; ni watu wakatili na wasio na huruma. Vishindo vyao ni kama mvumo wa bahari, wamepanda farasi. Wamejipanga tayari kwa vita, dhidi yako wewe Babuloni!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

42 Wameshika pinde zao na mikuki; ni watu wakatili na wasio na huruma. Vishindo vyao ni kama mvumo wa bahari, wamepanda farasi. Wamejipanga tayari kwa vita, dhidi yako wewe Babuloni!

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

42 Wamejifunga pinde na mikuki; ni wakatili na hawana huruma. Wanatoa sauti kama bahari inayounguruma wanapoendesha farasi wao; wanakuja kama watu waliojipanga tayari kwa vita ili kukushambulia, ee Binti Babeli.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

42 Wamejifunga pinde na mikuki; ni wakatili na wasio na huruma. Wanatoa sauti kama bahari inayonguruma wanapoendesha farasi zao; wanakuja kama watu waliojipanga tayari kwa vita ili kukushambulia, ee Binti Babeli.

Tazama sura Nakili




Yeremia 50:42
23 Marejeleo ya Msalaba  

Mataifa yanaghadhibika na falme kutetemeka; Anatoa sauti yake, nchi inayeyuka.


Ulitafakari agano lako; Maana mahali kwenye giza katika nchi Kumejaa makao ya ukatili.


Yeye aliyewapiga mataifa kwa ghadhabu, Kwa mapigo yasiyokoma; Aliyewatawala mataifa kwa hasira, Ameadhibiwa asizuie mtu.


Haya, shuka, keti mavumbini, Ewe bikira, binti Babeli; Keti chini pasipo kiti cha enzi, Ewe binti wa Wakaldayo; Maana hutaitwa tena mwororo, mpenda anasa.


Nilikuwa nimekasirika na watu wangu, niliutia unajisi urithi wangu, nikawatia mkononi mwako; wewe hukuwatendea rehema; kwa wazee uliifanya nira yako kuwa nzito sana.


Mishale yao ni mikali, na pinde zao zote zimepindika; Kwato za farasi wao zitahesabika kama gumegume; Na gurudumu zao kama kisulisuli;


Nao watanguruma juu yao siku hiyo Kama ngurumo ya bahari; Na mtu akiitazama nchi, ataona giza na dhiki Nayo nuru imetiwa giza katika mawingu yake.


Wote wakupendao wamekusahau; hawakutafuti; maana nimekujeruhi kwa jeraha la adui, kwa adhabu ya mtu mkatili; kwa sababu ya ukubwa wa uovu wako, kwa sababu dhambi zako zilikuwa zimeongezeka.


Kwa sababu ya kishindo cha kukanyaga kwa kwato za farasi wake walio hodari, kwa sababu ya mwendo wa mbio mbio wa magari yake ya vita; kwa sababu ya mngurumo wa magurudumu yake, hao akina baba hawatazami nyuma ili kuwaangalia watoto wao, kwa kuwa mikono yao ni dhaifu;


Jipangeni juu ya Babeli pande zote, Ninyi nyote mpindao upinde; Mpigeni, msiuzuie hata mshale mmoja; Kwa maana amemtenda BWANA dhambi.


Kwa maana juu ya Babeli nitaamsha na kuleta kusanyiko la mataifa makubwa, toka nchi ya kaskazini; nao watajipanga juu yake; kutoka huko atatwaliwa; mishale yao itakuwa kama ya mtu shujaa aliye stadi; hakuna hata mmoja utakaorudi bure.


Itwekeni bendera katika nchi, pigeni tarumbeta kati ya mataifa, yawekeni mataifa tayari juu yake; ziiteni juu yake falme za Ararati, na Mini, na Ashkenazi; agizeni jemadari juu yake; wapandisheni farasi, kama tunutu.


Kutoka Dani kumesikiwa mkoromo wa farasi wake; nchi yote pia inatetemeka kwa sauti ya mlio wa farasi wake wa vita; maana wamekuja, wamekula nchi na vyote vilivyomo; huo mji na wote wakaao ndani yake.


basi Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, mimi ni juu yako, Ee Tiro, nami nitaleta mataifa mengi kupigana nawe, kama bahari iinuavyo mawimbi yake.


Kama mshindo wa magari ya vita juu ya vilele vya milima, ndivyo warukavyo; kama mshindo wa miali ya moto iunguzapo mabua makavu, kama mashujaa waliopangwa tayari kwa vita.


Maana hukumu haina huruma kwake yeye asiyeona huruma. Huruma hujitukuza juu ya hukumu.


kwa kuwa walimwaga damu ya watakatifu na ya manabii, nawe umewapa damu wainywe; ndiyo wanayostahili.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo