Yeremia 50:28 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC28 Sauti yao wakimbiao na kuokoka, Kutoka katika nchi ya Babeli, Ili kutangaza katika Sayuni kisasi cha BWANA, Mungu wetu, Kisasi cha hekalu lake. Tazama suraMatoleo zaidiBiblia Habari Njema28 “Sikiliza! Wakimbizi na watoro kutoka nchi ya Babuloni wanakuja kutangaza huko Siyoni jinsi Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, alivyolipiza kisasi kwa ajili ya hekalu lake. Tazama suraBiblia Habari Njema - BHND28 “Sikiliza! Wakimbizi na watoro kutoka nchi ya Babuloni wanakuja kutangaza huko Siyoni jinsi Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, alivyolipiza kisasi kwa ajili ya hekalu lake. Tazama suraBiblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza28 “Sikiliza! Wakimbizi na watoro kutoka nchi ya Babuloni wanakuja kutangaza huko Siyoni jinsi Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, alivyolipiza kisasi kwa ajili ya hekalu lake. Tazama suraNeno: Bibilia Takatifu28 Wasikilizeni watoro na wakimbizi kutoka Babeli wakitangaza katika Sayuni jinsi Mwenyezi Mungu, Mungu wetu alivyolipiza kisasi, kisasi kwa ajili ya Hekalu lake. Tazama suraNeno: Maandiko Matakatifu28 Wasikilizeni watoro na wakimbizi kutoka Babeli wakitangaza katika Sayuni jinsi bwana, Mungu wetu alivyolipiza kisasi, kisasi kwa ajili ya Hekalu lake. Tazama sura |
Bali umejiinua juu ya Bwana wa mbingu; nao wamevileta vyombo vya nyumba yake mbele yako; na wewe, na wakuu wako, na wake zako, na masuria wako, mmevinywea; nawe umeisifu miungu ya fedha na ya dhahabu na ya shaba, na ya chuma, na ya mti, na ya mawe; wasioona, wala kusikia, wala kujua neno lolote; na Mungu yule, ambaye pumzi yako i mkononi mwake, na njia zako zote ni zake, hukumtukuza.