Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 50:25 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

25 BWANA amefungua akiba yake ya silaha, naye amezitoa silaha za ghadhabu yake; maana Bwana, BWANA wa majeshi, ana kazi atakayofanya katika nchi ya Wakaldayo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

25 Nimefungua ghala yangu ya silaha, nikatoa humo silaha za ghadhabu yangu, maana mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nina kazi ya kufanya katika nchi ya Wakaldayo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

25 Nimefungua ghala yangu ya silaha, nikatoa humo silaha za ghadhabu yangu, maana mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nina kazi ya kufanya katika nchi ya Wakaldayo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

25 Nimefungua ghala yangu ya silaha, nikatoa humo silaha za ghadhabu yangu, maana mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nina kazi ya kufanya katika nchi ya Wakaldayo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

25 Mwenyezi Mungu amefungua ghala lake la silaha na kuzitoa silaha za ghadhabu yake, kwa kuwa Bwana Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, anayo kazi ya kufanya katika nchi ya Wakaldayo.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

25 bwana amefungua ghala lake la silaha na kuzitoa silaha za ghadhabu yake, kwa kuwa bwana Mwenyezi Mwenye Nguvu Zote anayo kazi ya kufanya katika nchi ya Wakaldayo.

Tazama sura Nakili




Yeremia 50:25
17 Marejeleo ya Msalaba  

Jifungie upanga wako pajani, wewe uliye hodari, Utukufu ni wako na fahari ni yako.


Mishale yako ni mikali, katika mioyo ya adui za mfalme; Watu huanguka chini yako.


Kila mtu atakayeonekana atatumbuliwa, na kila mtu atakayepatikana ataanguka kwa upanga.


Mpigieni kelele pande zote; amejitoa; Maboma yake yameanguka, kuta zake zimebomolewa; Kwa maana ni kisasi cha BWANA; mlipizeni kisasi; Kama yeye alivyotenda, mtendeni yeye.


Wewe ni rungu langu na silaha zangu za vita; kwa wewe nitawavunjavunja mataifa; na kwa wewe nitaharibu falme;


Tazama, mimi niko juu yako, Ee mlima uharibuo, asema BWANA; wewe uiharibuye dunia nzima; nami nitaunyosha mkono wangu juu yako, na kukubingirisha chini toka majabalini; nami nitakufanya kuwa mlima ulioteketezwa.


Maana BWANA amwangamiza Babeli, Na kuikomesha sauti kuu ndani yake; Na mawimbi yake yavuma kama maji mengi, Mshindo wa sauti zao wafanya makelele;


Je! Tarumbeta itapigwa mjini, watu wasiogope? Mji utapatikana na hali mbaya, asiyoileta BWANA?


Kwa sababu hiyo mapigo yake yatakuja katika siku moja, mauti, na huzuni, na njaa, naye atateketezwa kabisa kwa moto. Kwa maana Bwana Mungu aliyemhukumu ni mwenye nguvu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo