Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 50:24 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

24 Nimekutegea mtego, Ee Babeli, nawe ukanaswa, nawe ulikuwa huna habari; umeonekana, ukakamatwa, kwa sababu ulishindana na BWANA.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

24 Ewe Babuloni, nilikutegea mtego ukanaswa, wala hukujua juu yake; ulipatikana, ukakamatwa, kwa sababu ulishindana nami Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

24 Ewe Babuloni, nilikutegea mtego ukanaswa, wala hukujua juu yake; ulipatikana, ukakamatwa, kwa sababu ulishindana nami Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

24 Ewe Babuloni, nilikutegea mtego ukanaswa, wala hukujua juu yake; ulipatikana, ukakamatwa, kwa sababu ulishindana nami Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

24 Nimetega mtego kwa ajili yako, ee Babeli, nawe ukakamatwa kabla hujafahamu; ulipatikana na ukakamatwa kwa sababu ulimpinga Mwenyezi Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

24 Nimetega mtego kwa ajili yako, ee Babeli, nawe ukakamatwa kabla haujafahamu; ulipatikana na ukakamatwa kwa sababu ulimpinga bwana.

Tazama sura Nakili




Yeremia 50:24
17 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa kuwa amenyosha mkono wake juu ya Mungu, Na kuendelea kwa kiburi kinyume cha Mwenyezi;


Je! Mwenye hoja atashindana na Mwenyezi? Mwenye kujadiliana na Mungu, na ajibu yeye.


Au je! Wewe una mkono kama Mungu? Waweza kutoa ngurumo kwa sauti kama yeye?


Yeye ni mwenye hekima moyoni, na mwenye uwezo katika nguvu; Ni nani aliyejifanya kuwa mgumu juu yake, naye akafanikiwa?


Basi Musa na Haruni wakaingia kwa Farao, na kumwambia, BWANA, Mungu wa Waebrania, asema hivi, Je! Utakataa hata lini kujinyenyekeza mbele zangu? Wape watu wangu ruhusa waende zao, ili wanitumikie.


Maana mwanadamu naye hajui wakati wake; kama samaki wanaokamatwa katika nyavu mbaya, na mfano wa ndege wanaonaswa mtegoni, kadhalika wanadamu hunaswa katika wakati mbaya, unapowaangukia kwa ghafla.


Nami nitaadhibu ulimwengu kwa sababu ya ubaya wake, na wenye dhambi kwa sababu ya hatia yao; nami nitaikomesha fahari yao wenye kiburi; nami nitayashusha chini majivuno yao walio wakali;


Ole wake ashindanaye na Muumba wake! Kigae kimoja katika vigae vya dunia! Je! Udongo umwambie yeye aufinyangaye; Unatengeneza nini? Au chombo ulichotengeneza hakina mikono?


Hofu, na shimo, na mtego, zaja juu yako, Ee mwenyeji wa Moabu, asema BWANA.


Aikimbiaye hofu ataanguka shimoni; na yeye atokaye shimoni atanaswa kwa mtego; maana nitaleta juu yake, yaani, juu ya Moabu, mwaka wa kujiliwa kwake, asema BWANA.


Nami nitawalevya wakuu wake, na watu wake wenye hekima, watawala wake, na makamanda wake, na mashujaa wake; nao watalala usingizi wa milele, wasiamke, asema Mfalme, BWANA wa majeshi, ambaye jina lake ni BWANA.


Babeli umeanguka na kuangamia ghafla; mwombolezeni; twaeni zeri kwa maumivu yake; ili labda apate kuponywa.


yule mpingamizi, ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama cha kuabudiwa; hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la Mungu, akijionesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo