Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yeremia 50:21 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

21 Panda juu ya nchi ya Merathaimu, naam, juu yake, na juu yao wakaao Pekodi; ua, ukaangamize nyuma yao, asema BWANA, ukatende kama nilivyokuagiza, yote pia.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

21 “Pandeni, mwiendee nchi ya Merathaimu, nendeni kuishambulia; washambulieni wakazi wa Pekodi na kuwaangamiza kabisa watu wake. Nasema mimi Mwenyezi-Mungu. Fanyeni kila kitu nilichowaamuru.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

21 “Pandeni, mwiendee nchi ya Merathaimu, nendeni kuishambulia; washambulieni wakazi wa Pekodi na kuwaangamiza kabisa watu wake. Nasema mimi Mwenyezi-Mungu. Fanyeni kila kitu nilichowaamuru.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

21 “Pandeni, mwiendee nchi ya Merathaimu, nendeni kuishambulia; washambulieni wakazi wa Pekodi na kuwaangamiza kabisa watu wake. Nasema mimi Mwenyezi-Mungu. Fanyeni kila kitu nilichowaamuru.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

21 “Shambulieni nchi ya Merathaimu na wale wanaoishi huko Pekodi. Wafuatieni, waueni na kuwaangamiza kabisa,” asema Mwenyezi Mungu. “Fanyeni kila kitu nilichowaamuru.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

21 “Shambulieni nchi ya Merathaimu na wale waishio huko Pekodi. Wafuatieni, waueni na kuwaangamiza kabisa,” asema bwana. “Fanyeni kila kitu nilichowaamuru.

Tazama sura Nakili




Yeremia 50:21
17 Marejeleo ya Msalaba  

Daudi akamwambia Abishai, na watumishi wake wote, Angalieni, huyu mwanangu, aliyetoka viunoni mwangu, anautafuta uhai wangu; sembuse Mbenyamini huyu? Mwacheni alaani, kwa sababu BWANA ndiye aliyemwagiza.


Je! Nimepanda mimi, ili kupigana na mahali hapa na kupaangamiza, bila shauri la BWANA? BWANA ndiye aliyeniambia, Panda upigane na nchi hii na kuiangamiza.


Koreshi, mfalme wa Uajemi asema hivi; BWANA, Mungu wa mbinguni, amenipa falme zote za dunia; naye ameniagiza nimjengee nyumba katika Yerusalemu, ulioko Yuda. Basi kila mtu katika ninyi nyote mlio watu wake, BWANA, Mungu wake, na awe pamoja naye, na akwee.


Nitamtuma juu ya taifa lenye kukufuru, nitampa maagizo juu ya watu wa ghadhabu yangu, ateke nyara, na kuchukua mateka, na kuwakanyaga kama matope ya njiani.


nimwambiaye Koreshi, Mchungaji wangu, naye atayatenda mapenzi yangu; hata ataunena Yerusalemu, Utajengwa; na hilo hekalu, Msingi wako utawekwa.


Kusanyikeni, ninyi nyote, mkasikie; ni nani miongoni mwao aliyehubiri haya? BWANA amempenda; atatimiza mapenzi yake juu ya Babeli, na mkono wake utakuwa juu ya Wakaldayo.


Mimi, naam, mimi, nimenena; naam, nimemwita; nimemleta, naye ataifanikisha njia yake.


Tazama, nitawapa amri yangu, asema BWANA, na kuwarejesha kwenye mji huu; nao watapigana nao, na kuutwaa, na kuuteketeza kwa moto; nami nitaifanya miji ya Yuda kuwa ukiwa, isikaliwe na mtu.


Na alaaniwe mtu afanyaye kazi ya BWANA kwa ulegevu; na alaaniwe auzuiaye upanga wake usimwage damu.


Mpigieni kelele pande zote; amejitoa; Maboma yake yameanguka, kuta zake zimebomolewa; Kwa maana ni kisasi cha BWANA; mlipizeni kisasi; Kama yeye alivyotenda, mtendeni yeye.


Maana toka kaskazini taifa linakuja juu yake, litakaloifanya nchi yake kuwa ukiwa; wala hakuna mtu atakayekaa humo; wamekimbia, wamekwenda zao, mwanadamu na mnyama pia.


Kwa maana juu ya Babeli nitaamsha na kuleta kusanyiko la mataifa makubwa, toka nchi ya kaskazini; nao watajipanga juu yake; kutoka huko atatwaliwa; mishale yao itakuwa kama ya mtu shujaa aliye stadi; hakuna hata mmoja utakaorudi bure.


watu wa Babeli, na Wakaldayo wote, Pekodi na Shoa na Koa, na Waashuri wote pamoja nao; vijana wa kutamanika, wote pia, watawala na mawaziri, wakuu, na watu wenye sifa, wote wenye kupanda farasi.


Mungu wa milele ndiye makazi yako, Na mikono ya milele i chini yako. Na mbele yako amemsukumia mbali adui; Akasema, Angamiza.


Basi sasa nenda ukawapige Waamaleki, na kuviharibu kabisa vitu vyote walivyonavyo, wala msiwaachilie; bali waueni, mwanamume na mwanamke, na mtoto anyonyaye, ng'ombe na kondoo, ngamia na punda.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo