Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yeremia 50:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

13 Kwa sababu ya ghadhabu ya BWANA haitakaliwa na mtu, bali itakuwa ukiwa mtupu; kila mtu apitaye karibu na Babeli atashangaa, atazomea kwa sababu ya mapigo yake yote.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

13 Kwa sababu ya ghadhabu yangu Mwenyezi-Mungu, Babuloni haitakaliwa kabisa na watu, bali itakuwa jangwa kabisa; kila atakayepita karibu nayo atashangaa ataizomea kwa sababu ya majeraha yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

13 Kwa sababu ya ghadhabu yangu Mwenyezi-Mungu, Babuloni haitakaliwa kabisa na watu, bali itakuwa jangwa kabisa; kila atakayepita karibu nayo atashangaa ataizomea kwa sababu ya majeraha yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

13 Kwa sababu ya ghadhabu yangu Mwenyezi-Mungu, Babuloni haitakaliwa kabisa na watu, bali itakuwa jangwa kabisa; kila atakayepita karibu nayo atashangaa ataizomea kwa sababu ya majeraha yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

13 Kwa sababu ya hasira ya Mwenyezi Mungu hatakaliwa na mtu, lakini ataachwa ukiwa kabisa. Wote watakaopita Babeli watatiwa hofu na kudhihaki kwa sababu ya majeraha yake yote.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

13 Kwa sababu ya hasira ya bwana hatakaliwa na mtu, lakini ataachwa ukiwa kabisa. Wote watakaopita Babeli watatiwa hofu na kudhihaki kwa sababu ya majeraha yake yote.

Tazama sura Nakili




Yeremia 50:13
18 Marejeleo ya Msalaba  

Watu watampigia makofi, Na kumzomea atoke mahali pake.


ili kufanya nchi yao kuwa kitu cha kushangaza, na cha kuzomewa daima; kila mtu apitaye karibu nayo atashangaa, na kutikisa kichwa chake.


Nami nitaufanya mji huu kuwa kitu cha kushangaza watu, na kuzomewa; kila mtu apitaye karibu nao atashangaa, na kuzomea kwa sababu ya mapigo yake.


Na itakuwa miaka hiyo sabini itakapotimia, nitamwadhibu mfalme wa Babeli, na taifa lile, asema BWANA, kwa sababu ya uovu wao, na nchi ya Wakaldayo pia; nami nitaifanya kuwa ukiwa wa milele.


Tazama, nitawapa amri yangu, asema BWANA, na kuwarejesha kwenye mji huu; nao watapigana nao, na kuutwaa, na kuuteketeza kwa moto; nami nitaifanya miji ya Yuda kuwa ukiwa, isikaliwe na mtu.


Na Edomu atakuwa ajabu; kila mtu apitaye atashangaa, na kuzomea, kwa sababu ya mapigo yake yote.


Maana toka kaskazini taifa linakuja juu yake, litakaloifanya nchi yake kuwa ukiwa; wala hakuna mtu atakayekaa humo; wamekimbia, wamekwenda zao, mwanadamu na mnyama pia.


Wala hawatatwaa kwako jiwe moja liwe la pembeni, wala jiwe moja liwe msingi; bali wewe utakuwa ukiwa daima, asema BWANA.


Nayo nchi yatetemeka, nayo ina uchungu; maana makusudi ya BWANA juu ya Babeli yasimama, kuifanya nchi ya Babeli ukiwa, isikaliwe na mtu.


Na Babeli utakuwa magofu, makao ya mbwamwitu, ajabu, na mazomeo, pasipo mtu wa kukaa huko.


ukaseme, Ee BWANA, umenena kuhusu mji huu kwamba utakatiliwa mbali, usikaliwe na awaye yote, wala wanadamu wala wanyama, lakini uwe ukiwa hata milele.


Wafanya biashara kati ya makabila ya watu wakuzomea; umekuwa kitu cha kutisha, wala hutakuwapo tena milele.


Huu ndio mji ule wa furaha, Uliokaa salama, Uliosema moyoni mwake, Mimi niko, Wala hapana mwingine ila mimi. Jinsi ulivyokuwa ukiwa, Mahali pa kulala pa wanyama wa bara! Kila mtu apitaye atazomea, Na kutikisa mkono wake.


Nami ninayakasirikia sana mataifa yanayostarehe; kwa maana mimi nilikuwa nimekasirika kidogo tu, nao wakayazidisha maafa.


Na kizazi cha baadaye, wanenu watakaoinuka baada yenu, na mgeni atakayekuja kutoka nchi ya mbali, watasema, watakapoyaona mapigo ya nchi ile, na magonjwa aliyoitia BWANA;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo