Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 5:8 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

8 Walikuwa kama farasi walioshiba wakati wa asubuhi; kila mmoja akalia kwa kutamani mke wa mwenzake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

8 Walikuwa kama farasi walioshiba wenye tamaa, kila mmoja akimtamani mke wa jirani yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

8 Walikuwa kama farasi walioshiba wenye tamaa, kila mmoja akimtamani mke wa jirani yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

8 Walikuwa kama farasi walioshiba wenye tamaa, kila mmoja akimtamani mke wa jirani yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

8 Wamelishwa vizuri, kama farasi dume wenye tamaa nyingi, kila mmoja akimlilia mke wa mwanaume mwingine.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

8 Wamelishwa vizuri, kama farasi waume wenye tamaa nyingi, kila mmoja akimlilia mke wa mwanaume mwingine.

Tazama sura Nakili




Yeremia 5:8
15 Marejeleo ya Msalaba  

Hakuna mkuu katika nyumba hii kuliko mimi, wala hakunizuilia kitu chochote ila wewe, kwa kuwa wewe u mkewe. Nifanyeje ubaya huu mkubwa nimkosee Mungu?


Kama moyo wangu ulishawishwa kwa mwanamke, Nami nimeotea mlangoni pa jirani yangu;


Usiitamani nyumba ya jirani yako, usimtamani mke wa jirani yako; wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng'ombe wake, wala punda wake, wala chochote alicho nacho jirani yako.


Ndivyo alivyo aingiaye kwa mke wa jirani yake; Kila mtu amgusaye huyo atakuwa na hatia.


Nimeona machukizo yako, naam, uzinifu wako, na ubembe wako, na uasherati wa ukahaba wako, juu ya milima katika mashamba. Ole wako, Ee Yerusalemu! Hutaki kutakaswa; mambo hayo yataendelea hata lini?


Maana nchi imejaa wazinzi; kwa sababu ya kuapa nchi inaomboleza; malisho ya nyikani yamekauka; mwenendo wao ni mbaya, na nguvu zao si za haki.


kwa sababu wametenda upumbavu katika Israeli, nao wamezini na wake za jirani zao, nao wamenena maneno ya uongo kwa jina langu, nisiyowaamuru; nami ndimi nijuaye, nami ni shahidi, asema BWANA.


Kwa sababu mnafurahi, kwa sababu mnashangilia, enyi mnaouteka urithi wangu, kwa sababu mmenona kama mtamba akanyagaye nafaka, nanyi mnalia kama farasi wenye nguvu;


Laiti ningekuwa na mahali pa kukaa jangwani, kibanda cha wasafiri; nipate kuwaacha watu wangu, na kuondoka kwao! Maana wao ni wazinzi, wote pia, mkutano wa watu wenye hiana.


Na mtu mmoja amefanya chukizo pamoja na mke wa jirani yake; na mtu mwingine amemharibu mke wa mwanawe kwa uasherati; na mtu mwingine ndani yako amemfanyia nguvu dada yake, binti ya babaye.


Wala usimtamani mke wa jirani yako; wala usiitamani nyumba ya jirani yako, wala shamba lake, wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng'ombe wake, wala punda wake, wala kitu chochote alicho nacho jirani yako.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo