Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 5:22 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

22 Je! Hamniogopi mimi? Asema BWANA; hamtatetemeka mbele za uso wangu; mimi niliyeweka mchanga kuwa mpaka wa bahari, kwa amri ya daima, isiweze kuupita? Mawimbi yake yajapoumuka-umuka, hayawezi kushinda nguvu; yajapovuma sana, hayawezi kuupita.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

22 Mbona hamniogopi? Nauliza mimi Mwenyezi-Mungu! Kwa nini hamtetemeki mbele yangu? Mimi niliweka mchanga uwe mpaka wa bahari, kizuizi cha daima ambacho bahari haiwezi kuvuka. Ingawa mawimbi yanaupiga, hayawezi kuupita; ingawa yananguruma, hayawezi kuuruka.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

22 Mbona hamniogopi? Nauliza mimi Mwenyezi-Mungu! Kwa nini hamtetemeki mbele yangu? Mimi niliweka mchanga uwe mpaka wa bahari, kizuizi cha daima ambacho bahari haiwezi kuvuka. Ingawa mawimbi yanaupiga, hayawezi kuupita; ingawa yananguruma, hayawezi kuuruka.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

22 Mbona hamniogopi? Nauliza mimi Mwenyezi-Mungu! Kwa nini hamtetemeki mbele yangu? Mimi niliweka mchanga uwe mpaka wa bahari, kizuizi cha daima ambacho bahari haiwezi kuvuka. Ingawa mawimbi yanaupiga, hayawezi kuupita; ingawa yananguruma, hayawezi kuuruka.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

22 Je, haiwapasi kuniogopa mimi?” asema Mwenyezi Mungu. “Je, haiwapasi kutetemeka mbele zangu? Niliufanya mchanga kuwa mpaka wa bahari, kizuizi cha milele ambacho bahari haiwezi kuupita. Mawimbi yanaweza kuumuka, lakini hayawezi kuupita; yanaweza kunguruma, lakini hayawezi kuuvuka.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

22 Je, haiwapasi kuniogopa mimi?” asema bwana. “Je, haiwapasi kutetemeka mbele zangu? Niliufanya mchanga kuwa mpaka wa bahari, kizuizi cha milele ambacho haiwezi kupita. Mawimbi yanaweza kuumuka, lakini hayawezi kuupita; yanaweza kunguruma, lakini hayawezi kuuvuka.

Tazama sura Nakili




Yeremia 5:22
29 Marejeleo ya Msalaba  

Mungu akasema, Maji yaliyo chini ya mbingu na yakusanyike mahali pamoja, ili pakavu paonekane; ikawa hivyo.


Akaenda, akamwona yule maiti ametupwa njiani, na punda na simba wamesimama karibu na maiti; yule simba alikuwa hakumla maiti, wala hakumrarua punda.


Amepiga duara kuwa ni mpaka juu ya uso wa maji, Hata hapo mwanga na giza vinapopakana.


Kwa hiyo watu humwogopa; Yeye hawaangalii walio na hekima mioyoni.


Au ni nani aliyeifunga bahari kwa milango, Hapo ilipotoka kwa nguvu kama kwamba imetoka tumboni mwa nchi.


Umeweka mpaka yasiupite, Wala yasirudi kuifunikiza nchi.


Mwili wangu unatetemeka kwa kukucha Wewe, Nami ninaziogopa hukumu zako.


Hukusanya maji ya bahari chungu chungu, Huviweka vilindi katika ghala.


Maji yake yajapovuma na kuumuka, Ijapopepesuka milima kwa kiburi chake.


BWANA ametamalaki, mataifa wanatetemeka; Ameketi juu ya makerubi, nchi inatikisika.


Alipoipa bahari mpaka wake, Kwamba maji yake yasiasi amri yake; Alipoiagiza misingi ya nchi;


Basi, nilipokuja, mbona hapakuwa na mtu? Nilipoita, mbona hapakuwa na mtu aliyenijibu? Je! Mkono wangu ni mfupi, hata nisiweze kukomboa? Au je! Mimi sina nguvu za kuponya? Tazama, kwa kukemea kwangu naikausha bahari, mito ya maji naifanya kuwa jangwa; samaki wao wanuka kwa sababu hapana maji, nao wafa kwa kiu.


kama vile moto uchomapo vichaka, na moto uchemshapo maji; ili kuwajulisha adui zako jina lako, mataifa wakatetemeke mbele zako!


Lisikilizeni neno la BWANA, ninyi mtetemekao kwa sababu ya neno lake; Ndugu zenu wawachukiao ninyi, waliowatupa kwa ajili ya jina langu, wamesema, Na atukuzwe BWANA, tupate kuiona furaha yenu; lakini watatahayarika.


Ni nani asiyekucha wewe, Ee mfalme wa mataifa? Maana hii ni sifa yako wewe; kwa kuwa miongoni mwa wenye hekima wote wa mataifa, na katika hali yao ya enzi yote pia, hapana hata mmoja kama wewe.


Uovu wako mwenyewe utakurudi, maasi yako yatakukaripia; ujue, basi, ukaone, ya kuwa ni jambo baya sana na uchungu, kuwa umemwacha BWANA, Mungu wako, na ya kuwa moyoni mwako hamna kunihofu, asema Bwana, BWANA wa majeshi.


BWANA asema hivi, awapaye watu jua, ili kuwa nuru wakati wa mchana, na amri za mwezi na nyota, ili kuwa nuru wakati wa usiku, aichafuaye bahari, hata mawimbi yake yakavuma; BWANA wa majeshi, ndilo jina lake;


Mimi ninaweka amri, ya kwamba katika mamlaka yote ya ufalme wangu watu watetemeke na kuogopa mbele za Mungu wa Danieli; maana yeye ndiye Mungu aliye hai, adumuye milele, na ufalme wake ni ufalme usioharibika, na mamlaka yake itadumu hata mwisho.


Basi nitakutenda hivi, Ee Israeli, na kwa sababu nitakutenda hivi, ujiweke tayari kuonana na Mungu wako, Ee Israeli.


Yeye ndiye avijengaye vyumba vyake mbinguni, na kuweka misingi ya kuba yake juu ya nchi; yeye ndiye ayaitaye maji ya bahari, na kuyamwaga juu ya uso wa nchi; BWANA ndilo jina lake.


Ndipo wale watu wakamwogopa BWANA mno, wakamtolea BWANA sadaka, na kuweka nadhiri.


Yeye huikemea bahari na kuikausha, pia huikausha mito yote; Bashani hulegea, na Karmeli; nalo ua la Lebanoni hulegea.


Msiwaogope wauuao mwili, wasiweze kuiua na roho; afadhali mwogopeni yule awezaye kuangamiza mwili na roho pia katika Jehanamu.


Akaamka, akaukemea upepo, akaiambia bahari, Nyamaza, utulie. Upepo ukakoma, kukawa shwari kuu.


Lakini nitawaonya mtakayemwogopa; mwogopeni yule ambaye akiisha kumwua mtu ana uweza wa kumtupa katika Jehanamu; naam, nawaambia, Mwogopeni huyo.


Kama hutaki kutunza kufanya maneno yote ya torati hii yaliyoandikwa katika kitabu hiki, upate kulicha jina hili la fahari na utisho, BWANA, MUNGU WAKO;


Ni nani asiyekucha, Ee Bwana, na kulitukuza jina lako? Kwa kuwa wewe peke yako u Mtakatifu; kwa maana mataifa yote watakuja na kusujudu mbele zako; kwa kuwa matendo yako ya haki yamekwisha kufunuliwa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo