Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 5:19 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

19 Tena itakuwa mtakapouliza, BWANA ametutenda mambo hayo yote kwa sababu gani? Ndipo utakapowaambia, Vile vile kama ninyi mlivyoniacha mimi, na kuwatumikia miungu mingine katika nchi yenu wenyewe, ndivyo mtakavyowatumikia wageni katika nchi isiyo yenu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

19 Na watu wenu watakapouliza ‘Kwa nini Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, ametutendea mambo hayo yote?’ Wewe utawaambia, ‘Nyinyi mlimwacha Mwenyezi-Mungu, mkaitumikia miungu ya kigeni katika nchi yenu. Basi ndivyo mtakavyowatumikia watu wengine katika nchi isiyo yenu.’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

19 Na watu wenu watakapouliza ‘Kwa nini Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, ametutendea mambo hayo yote?’ Wewe utawaambia, ‘Nyinyi mlimwacha Mwenyezi-Mungu, mkaitumikia miungu ya kigeni katika nchi yenu. Basi ndivyo mtakavyowatumikia watu wengine katika nchi isiyo yenu.’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

19 Na watu wenu watakapouliza ‘Kwa nini Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, ametutendea mambo hayo yote?’ Wewe utawaambia, ‘Nyinyi mlimwacha Mwenyezi-Mungu, mkaitumikia miungu ya kigeni katika nchi yenu. Basi ndivyo mtakavyowatumikia watu wengine katika nchi isiyo yenu.’

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

19 “Nao watu watakapouliza, ‘Kwa nini Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, ametufanyia mambo haya yote?’ utawaambia, ‘Kama mlivyoniacha mimi kwa kuitumikia miungu migeni katika nchi yenu wenyewe, ndivyo sasa mtakavyowatumikia wageni katika nchi ambayo si yenu.’

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

19 “Nao watu watakapouliza, ‘Kwa nini bwana, Mungu wetu ametufanyia mambo haya yote?’ utawaambia, ‘Kama vile mlivyoniacha mimi na kutumikia miungu migeni katika nchi yenu wenyewe, ndivyo sasa mtakavyowatumikia wageni katika nchi ambayo si yenu.’

Tazama sura Nakili




Yeremia 5:19
18 Marejeleo ya Msalaba  

Nawe ukisema moyoni mwako, Mbona mambo haya yamenipata mimi? Ni kwa sababu ya wingi wa uovu wako, marinda yako yamefunuliwa, na visigino vya miguu yako vimeumia.


basi, kwa sababu hiyo, nitawatoeni katika nchi hii, na kuwaingiza katika nchi ambayo hamkuijua, wala ninyi wala baba zenu; na huko mtawatumikia miungu mingine mchana na usiku; kwa maana mimi sitawapa fadhili zangu hata kidogo.


Nawe, naam, wewe nafsi yako, utaachana na urithi wako niliokupa; nami nitakulazimisha kuwatumikia adui zako katika nchi usiyoijua; maana umewasha moto katika hasira yangu, utakaowaka milele.


Kwa maana watu wangu hawa wametenda maovu mawili; wameniacha mimi, niliye chemchemi ya maji ya uzima, wamejichimbia visima, visima vyenye nyufa visivyoweza kuweka maji.


Je! Israeli ni mtumwa? Je! Ni mzalia? Mbona amekuwa mateka?


Lakini ulisema, Sina hatia mimi; bila shaka hasira yake imegeuka na kuniacha. Tazama, nitaingia hukumuni pamoja nawe, kwa sababu unasema, Sikutenda dhambi mimi.


Lakini hata katika siku zile, asema BWANA, sitawakomesha ninyi kabisa.


Tangazeni neno hili katika nyumba ya Yakobo, litangazeni katika Yuda, kusema,


Ni nani aliye na hekima, apate kuelewa haya? Tena ni nani ambaye kinywa cha BWANA kimesema naye, apate kuyatangaza? Nayo ni nini maana yake nchi hii kuharibika, na kuteketea kama nyika, asipite mtu?


Naye BWANA asema, Ni kwa sababu wameiacha sheria yangu niliyoweka mbele yao, wala hawakuitii sauti yangu, wala kuenda katika hiyo;


Watumwa wanatutawala; Hakuna mtu wa kutuokoa na mikono yao.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo