Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 49:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

5 Tazama, nitaleta hofu juu yako, asema Bwana, BWANA wa majeshi, itakayotoka kwa wote wakuzungukao; nanyi mtafukuzwa nje, kila mtu mbali kabisa, wala hapana mtu wa kuwakusanya wapoteao.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 Basi, mimi nitawaleteeni vitisho kutoka kwa jirani zenu wote, nanyi mtafukuzwa nje kila mtu kivyake, bila mtu wa kuwakusanya wakimbizi. Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nimesema.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 Basi, mimi nitawaleteeni vitisho kutoka kwa jirani zenu wote, nanyi mtafukuzwa nje kila mtu kivyake, bila mtu wa kuwakusanya wakimbizi. Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nimesema.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 Basi, mimi nitawaleteeni vitisho kutoka kwa jirani zenu wote, nanyi mtafukuzwa nje kila mtu kivyake, bila mtu wa kuwakusanya wakimbizi. Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nimesema.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 Nitaleta hofu kuu juu yako kutoka kwa wale wote wanaokuzunguka,” asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni. “Kila mmoja wenu ataondolewa, wala hakuna hata mmoja atakayekusanya wakimbizi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 Nitaleta hofu kuu juu yako kutoka kwa wale wote wanaokuzunguka,” asema Bwana, bwana Mwenye Nguvu Zote. “Kila mmoja wenu ataondolewa, wala hakuna hata mmoja atakayekusanya wakimbizi.

Tazama sura Nakili




Yeremia 49:5
16 Marejeleo ya Msalaba  

Tazama, nitatia roho ya hofu ndani yake, naye atasikia uvumi, na kuirudia nchi yake mwenyewe; nami nitamwangusha kwa upanga katika nchi yake mwenyewe.


Sauti za utisho zi masikioni mwake; Katika kufanikiwa kwake mtekaji nyara atamjia juu yake;


Waovu hukimbia wasipofuatiwa na mtu; Bali wenye haki ni wajasiri kama simba.


Lete shauri; kata neno; fanya kivuli chako kuwa kama usiku kati ya mchana; wafiche waliofukuzwa; usiwachongee waliopotea.


Wajane wao wameongezeka kwangu kuliko mchanga wa bahari; nimeleta mwenye kuteka wakati wa adhuhuri juu ya mama wa vijana; nimeleta uchungu na hofu kuu impate ghafla.


Tazama, asema BWANA, Nitatuma watu kuwaita wavuvi wengi, nao watawavua; na baada ya hayo nitatuma watu kuwaita wawindaji wengi, nao watawawinda, watoke katika kila mlima, na kila kilima, na pango za majabali.


Maana BWANA asema hivi, Tazama, nitakufanya kuwa hofu kuu kwa nafsi yako, na kwa rafiki zako wote; nao wataanguka kwa upanga wa adui zao, na macho yako yataona hayo; nami nitatia Yuda yote katika mikono ya mfalme wa Babeli, naye atawachukua mateka mpaka Babeli, na kuwaua kwa upanga.


Nimeyaona haya kwa sababu gani? Wamefadhaika, wamerudi nyuma; mashujaa wao wamevunjikavunjika; wanakimbia upesi sana, hawatazami nyuma; hofu iko pande zote; asema BWANA.


Hema zao na makundi yao watayatwaa; watachukulia mbali mapazia yao kwa faida yao wenyewe, na vyombo vyao vyote, na ngamia wao; nao watawapigia kelele wakisema, Hofu ziko pande zote.


Msitoke kwenda mashambani, wala msitembee njiani, kwa maana upanga wa adui uko huko; hofu ziko pande zote.


Watu waliwapigia kelele, Ondokeni, Uchafu, Ondokeni, ondokeni, msiguse; Walipokimbia na kutangatanga, watu walisema kati ya mataifa, Hawatakaa hapa tena.


Nanyi mtatoka kwenye mahali palipobomolewa, kila mwanamke moja kwa moja mbele yake; nanyi mtajitupa katika Harmoni, asema BWANA.


akawaambia wale wanaume, Mimi najua ya kuwa BWANA amewapa ninyi nchi hii, na ya kuwa hofu imetuangukia mbele yenu, na ya kuwa wenyeji wote wa nchi wanayeyuka mbele yenu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo