Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 49:33 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

33 Na Hazori utakuwa kao la mbwamwitu; ukiwa milele; hakuna mtu atakayekaa huko, wala hakuna mwanadamu atakayekaa huko kama mgeni akaavyo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

33 Mji wa Hazori utakuwa makao ya mbweha, utakuwa jangwa daima; hakuna mtu atakayekaa humo, wala atakayeishi humo.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

33 Mji wa Hazori utakuwa makao ya mbweha, utakuwa jangwa daima; hakuna mtu atakayekaa humo, wala atakayeishi humo.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

33 Mji wa Hazori utakuwa makao ya mbweha, utakuwa jangwa daima; hakuna mtu atakayekaa humo, wala atakayeishi humo.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

33 “Hazori itakuwa makao ya mbweha, mahali pa ukiwa milele. Hakuna atakayeishi humo; hakuna mtu atakayekaa ndani yake.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

33 “Hazori itakuwa makao ya mbweha, mahali pa ukiwa milele. Hakuna yeyote atakayeishi humo; hakuna mtu atakayekaa ndani yake.”

Tazama sura Nakili




Yeremia 49:33
13 Marejeleo ya Msalaba  

Tena nitaifanya hiyo nchi kuwa makao ya nungunungu, na maziwa ya maji; nami nitaifagilia mbali kwa ufagio wa uharibifu; asema BWANA wa majeshi.


Sauti imesikiwa, Tazama, inakuja; mshindo mkuu kutoka nchi ya kaskazini, ili kuifanya miji ya Yuda kuwa ukiwa, makao ya mbweha.


Na Babeli utakuwa magofu, makao ya mbwamwitu, ajabu, na mazomeo, pasipo mtu wa kukaa huko.


Nami nitafanya Yerusalemu kuwa magofu, Makao ya mbweha; Nami nitaifanya miji ya Yuda kuwa ukiwa, Isikaliwe na mtu awaye yote.


Basi kama niishivyo, asema BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, Hakika Moabu atakuwa kama Sodoma, na wana wa Amoni kama Gomora, yaani, milki ya upupu, na mashimo ya chumvi, ukiwa wa daima; watu wangu waliosalia watawateka nyara, na watu wa taifa langu waliobaki watawarithi.


bali Esau nimemchukia na kuifanya milima yake kuwa ukiwa, na urithi wake nimewapa mbweha wa nyikani.


Akalia kwa sauti kuu, akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli ulio mkuu; umekuwa maskani ya mashetani, na ngome ya kila roho mchafu, na ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo