Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Yeremia 49:30 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

30 Kimbieni ninyi, nendeni mbali mkitangatanga, kaeni chini sana, enyi mkaao Hazori, asema BWANA; maana Nebukadneza, mfalme wa Babeli, amefanya shauri juu yenu, naye amekusudia neno juu yenu.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

30 Kimbieni, nendeni mbali, kaeni mashimoni. Enyi wakazi wa Haziri, kimbieni mtangetange na kukaa mafichoni! Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema. Maana Nebukadneza mfalme wa Babuloni, amefanya mpango dhidi yenu, amepania kuja kuwashambulia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

30 Kimbieni, nendeni mbali, kaeni mashimoni. Enyi wakazi wa Haziri, kimbieni mtangetange na kukaa mafichoni! Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema. Maana Nebukadneza mfalme wa Babuloni, amefanya mpango dhidi yenu, amepania kuja kuwashambulia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

30 Kimbieni, nendeni mbali, kaeni mashimoni. Enyi wakazi wa Haziri, kimbieni mtangetange na kukaa mafichoni! Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema. Maana Nebukadneza mfalme wa Babuloni, amefanya mpango dhidi yenu, amepania kuja kuwashambulia.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

30 “Kimbieni haraka! Kaeni kwenye mapango marefu sana, ninyi mnaoishi Hazori,” asema Mwenyezi Mungu. “Nebukadneza, mfalme wa Babeli amepanga njama dhidi yenu; amebuni hila dhidi yenu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

30 “Kimbieni haraka! Kaeni kwenye mapango marefu sana, ninyi mkaao Hazori,” asema bwana. “Nebukadneza, mfalme wa Babeli amepanga shauri baya dhidi yenu; amebuni hila dhidi yenu.

Tazama sura Nakili

Yeremia 49:30
4 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini hivyo sivyo akusudiavyo mwenyewe, wala sivyo moyo wake uwazavyo; maana katika moyo wake akusudia kuharibu, na kukatilia mbali mataifa, wala si mataifa machache.

angalieni, nitatuma watu na kuzitwaa jamaa zote za upande wa kaskazini, asema BWANA, nami nitatuma ujumbe kwa Nebukadneza, mfalme wa Babeli, mtumishi wangu, nami nitawaleta juu ya nchi hii, na juu yao wakaao ndani yake, na juu ya mataifa haya yote yaliyoko pande zote; nami nitawaangamiza kabisa, na kuwafanya kitu cha kushangaza, na kitu cha kuzomewa, na ukiwa wa daima.

Na sasa nimetia nchi hizi zote katika mkono wa Nebukadneza, mfalme wa Babeli, mtumishi wangu; na wanyama pori pia nimempa wamtumikie.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo