Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 49:29 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

29 Hema zao na makundi yao watayatwaa; watachukulia mbali mapazia yao kwa faida yao wenyewe, na vyombo vyao vyote, na ngamia wao; nao watawapigia kelele wakisema, Hofu ziko pande zote.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

29 Hema zao na kondoo wao vitachukuliwa, kadhalika mapazia yao na mali yao yote; watanyanganywa ngamia wao, na kilio kitasikika: ‘Kitisho kila upande!’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

29 Hema zao na kondoo wao vitachukuliwa, kadhalika mapazia yao na mali yao yote; watanyanganywa ngamia wao, na kilio kitasikika: ‘Kitisho kila upande!’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

29 Hema zao na kondoo wao vitachukuliwa, kadhalika mapazia yao na mali yao yote; watanyang'anywa ngamia wao, na kilio kitasikika: ‘Kitisho kila upande!’

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

29 Mahema yao na makundi yao ya kondoo yatachukuliwa; vibanda vyao vitatwaliwa, pamoja na mali yao yote na ngamia wao. Watu watawapigia kelele, ‘Hofu kuu iko kila upande!’

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

29 Hema zao na makundi yao ya kondoo yatachukuliwa; vibanda vyao vitatwaliwa pamoja na mali zao zote na ngamia zao. Watu watawapigia kelele, ‘Hofu kuu iko kila upande!’

Tazama sura Nakili




Yeremia 49:29
21 Marejeleo ya Msalaba  

Nao wakakaa kitako kula chakula; wakainua macho yao, wakaona, msafara wa Waishmaeli wanakuja wakitoka Gileadi na ngamia zao, wakichukua ubani na zeri na manemane, wakisafiri kuvichukua mpaka Misri.


Mali yake nayo ilikuwa ni kondoo elfu saba, na ngamia elfu tatu, na jozi za ng'ombe mia tano, na punda wake mia tano, na watumishi wengi sana; basi hivi mtu huyo alikuwa ni mkuu sana kuliko watu wote wa upande wa mashariki.


Ole wangu mimi! Kwa kuwa ni mgeni katika Mesheki; Na kufanya makao yangu Katikati ya hema za Kedari.


Maana nimesikia wengi wakinong'onezana; Hofu katika pande zote. Waliposhauriana juu yangu, Walipanga kunitoa uhai wangu.


Hautakaliwa na watu tena kabisa, wala watu hawatakaa ndani yake tangu kizazi hata kizazi. Mwarabu hatapiga hema yake huko, wala wachungaji hawatalaza makundi yao huko.


Makundi yote ya Kedari yatakusanyika kwako, Kondoo dume wa Nebayothi watakutumikia; Watapanda juu ya madhabahu yangu kwa kibali, Nami nitaitukuza nyumba ya utukufu wangu.


Hema yangu imetekwa nyara, kamba zangu zote zimekatika; watoto wangu wameniacha na kwenda zao, pia hawako. Hakuna mtu atakayenitandikia tena hema yangu, na kuyatundika mapazia yangu.


Uangamivu baada ya uangamivu umetangazwa; kwa maana nchi yote imeharibika; hema zangu zimetekwa nyara ghafla, na mapazia yangu katika dakika moja.


Nimeyaona haya kwa sababu gani? Wamefadhaika, wamerudi nyuma; mashujaa wao wamevunjikavunjika; wanakimbia upesi sana, hawatazami nyuma; hofu iko pande zote; asema BWANA.


Dameski umedhoofika; Umejigeuza kukimbia; tetemeko limeushika; Dhiki na huzuni zimeupata, Kama za mwanamke katika uchungu wake.


Tazama, nitaleta hofu juu yako, asema Bwana, BWANA wa majeshi, itakayotoka kwa wote wakuzungukao; nanyi mtafukuzwa nje, kila mtu mbali kabisa, wala hapana mtu wa kuwakusanya wapoteao.


Msitoke kwenda mashambani, wala msitembee njiani, kwa maana upanga wa adui uko huko; hofu ziko pande zote.


Niliziona hema za Kushani zikitaabika; Mapazia ya nchi ya Midiani yakatetemeka.


Pande zote twateseka, bali hatusongwi; twaona shaka, bali hatukati tamaa;


Kwa maana hata tulipokuwa tumefika Makedonia miili yetu haikupata nafuu; bali tuliteseka kotekote; nje palikuwa na vita, ndani hofu.


Kwa maana walikwea na ng'ombe zao na hema zao, wakaja mfano wa nzige kwa wingi; wao na ngamia zao pia walikuwa hawana hesabu; nao waliingia katika hiyo nchi ili kuiharibu.


Nao Wamidiani na Waamaleki na, hao wana wa mashariki walikuwa wametua bondeni, mfano wa nzige kwa wingi; na ngamia wao walikuwa hawana hesabu; mfano wa mchanga wa ufuoni, kwa wingi.


Ndipo hapo Zeba na Salmuna wakasema, Simama wewe utuue sisi; kwa maana kama mtu alivyo, ndivyo zilivyo nguvu zake. Basi Gideoni akasimama, akawaua Zeba na Salmuna, akazitwaa koja zilizokuwa katika shingo za ngamia wao.


Na uzani wa hizo herini za dhahabu alizozitaka ulipata shekeli za dhahabu elfu moja na mia saba; mbali na makoja na vidani, na mavazi ya rangi ya zambarau waliyokuwa wameyavaa hao wafalme wa Midiani, tena mbali na mikufu iliyokuwa katika shingo za ngamia wao.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo