Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 49:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

2 Basi, kwa sababu hiyo, tazama, siku zinakuja, asema BWANA, nitakapofanya kishindo cha vita kisikike juu ya Raba, mji wa Amoni, nao utakuwa magofu ya ukiwa, na binti zake watateketezwa kwa moto; ndipo Israeli watawamiliki wao waliokuwa wakimmiliki, asema BWANA.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 Basi, wakati unakuja kweli, siku zaja, nasema mimi Mwenyezi-Mungu, ambapo nitavumisha sauti ya vita dhidi ya Raba mji wa Waamoni. Raba utakuwa rundo la uharibifu, vijiji vyake vitateketezwa moto; ndipo Israeli atakapowamiliki wale waliomiliki. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 Basi, wakati unakuja kweli, siku zaja, nasema mimi Mwenyezi-Mungu, ambapo nitavumisha sauti ya vita dhidi ya Raba mji wa Waamoni. Raba utakuwa rundo la uharibifu, vijiji vyake vitateketezwa moto; ndipo Israeli atakapowamiliki wale waliomiliki. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 Basi, wakati unakuja kweli, siku zaja, nasema mimi Mwenyezi-Mungu, ambapo nitavumisha sauti ya vita dhidi ya Raba mji wa Waamoni. Raba utakuwa rundo la uharibifu, vijiji vyake vitateketezwa moto; ndipo Israeli atakapowamiliki wale waliomiliki. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 Lakini siku zinakuja,” asema Mwenyezi Mungu, “nitakapopiga ukelele wa vita dhidi ya Raba, mji wa Waamoni; utakuwa kilima cha magofu, navyo vijiji vinavyouzunguka vitateketezwa kwa moto. Kisha Israeli atawafukuza wale waliomfukuza,” asema Mwenyezi Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 Lakini siku zinakuja,” asema bwana, “nitakapopiga kelele ya vita dhidi ya Raba mji wa Waamoni; utakuwa kilima cha magofu, navyo vijiji vinavyouzunguka vitateketezwa kwa moto. Kisha Israeli atawafukuza wale waliomfukuza,” asema bwana.

Tazama sura Nakili




Yeremia 49:2
22 Marejeleo ya Msalaba  

Hata ikawa, mwanzo wa mwaka mpya, wakati watokapo wafalme kwenda vitani, Daudi akamtuma Yoabu, na watumishi wake pamoja naye, na Israeli wote; wakawaangamiza Waamoni, wakauzingira Raba. Lakini Daudi mwenyewe akakaa Yerusalemu.


Na ufurahi mlima Sayuni. Binti za Yuda na washangilie Kwa sababu ya hukumu zako.


Sayuni imesikia na kufurahi, Binti za Yuda walishangilia, Kwa sababu ya hukumu zako, Ee BWANA.


Nao watashuka, watalirukia bega la Wafilisti upande wa magharibi; nao pamoja watawateka wana wa mashariki; watanyosha mkono juu ya Edomu na Moabu; na wana wa Amoni watawatii.


Ufunuo juu ya Dameski. Tazama, Dameski umeondolewa usiwe mji, nao utakuwa rundo la magofu.


Mtima wangu, mtima wangu! Naumwa katika moyo wangu wa ndani; moyo wangu umefadhaika ndani yangu; siwezi kunyamaza; kwa sababu umesikia, Ee nafsi yangu, sauti ya tarumbeta, mshindo wa vita.


Kuhusu wana wa Amoni. BWANA asema hivi, Je, Israeli hana wana? Je! Hana mrithi? Basi, mbona Malkamu anamiliki Gadi, na watu wake wanakaa katika miji yake?


Utachora njia, ili upanga upate kufikia Raba wa wana wa Amoni, na kufikia Yuda katika Yerusalemu, wenye maboma.


Na wewe, Ewe mtu mwovu, uliyetiwa jeraha kiasi cha kukuua, mkuu wa Israeli, ambaye siku yako imekuja, katika wakati wa uovu wa mwisho;


lakini nitawasha moto katika ukuta wa Raba, nao utayateketeza majumba yake; pamoja na kupiga kelele siku ya vita, pamoja na tufani katika siku ya chamchela;


Na watu wa Negebu wataumiliki mlima wa Esau; na watu wa Shefela watawamiliki Wafilisti; nao wataimiliki nchi ya Efraimu, na nchi ya Samaria, na Benyamini atamiliki Gileadi.


Tena hapo mtakapokwenda kupiga vita katika nchi yenu, kupigana na adui awaoneaye ninyi, ndipo mtakapopiga sauti ya kugutusha kwa tarumbeta; nanyi mtakumbukwa mbele za BWANA, Mungu wenu, nanyi mtaokolewa na adui zenu.


Basi Israeli wakaitwaa miji hiyo yote; Israeli wakakaa katika miji yote ya Waamori, katika Heshboni, na miji yake yote.


Na nyara zake zote uzikusanyie katikati ya njia yake; na mji uuteketeze kwa moto, na nyara zake zote, kuwe sadaka kamili ya kuteketezwa kwa BWANA, Mungu wako; nao utakuwa magofu milele; usijengwe tena.


(Kwani aliyesalia katika mabaki ya Warefai ni Ogu pekee, mfalme wa Bashani; tazama, kitanda chake kilikuwa kitanda cha chuma; kitanda hicho kingali kiko Raba kwa wana wa Amoni? Urefu wake ulikuwa ni dhiraa tisa, na upana wake dhiraa nane, kwa mfano wa mkono wa mtu).


Tena Manase alikuwa na miji katika Isakari na katika Asheri, nayo ni hii, Beth-sheani na vijiji vyake, Ibleamu na miji yake, wenyeji wa Dori na miji yake, wenyeji wa Endori na miji yake, wenyeji wa Taanaki na miji yake, wenyeji wa Megido na miji yake, na pia theluthi ya Nafathi.


Wana wa Yusufu wakasema, Hiyo nchi ya vilima haitutoshi sisi; lakini Wakanaani wote wakaao katika nchi ya bondeni wana magari ya chuma, hao walio katika Beth-sheani na miji yake, na hao walio katika bonde la Yezreeli pia.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo