Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 49:14 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

14 Nimepata habari kwa BWANA, Na mjumbe ametumwa kati ya mataifa, Akisema, Jikusanyeni, mkaujie, Mkainuke kwenda vitani.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Nimepata habari kutoka kwa Mwenyezi-Mungu, mjumbe ametumwa ayatangazie mataifa: “Jikusanyeni pamoja dhidi ya Edomu; inukeni mwende kuushambulia!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 Nimepata habari kutoka kwa Mwenyezi-Mungu, mjumbe ametumwa ayatangazie mataifa: “Jikusanyeni pamoja dhidi ya Edomu; inukeni mwende kuushambulia!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Nimepata habari kutoka kwa Mwenyezi-Mungu, mjumbe ametumwa ayatangazie mataifa: “Jikusanyeni pamoja dhidi ya Edomu; inukeni mwende kuushambulia!

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 Nimesikia ujumbe kutoka kwa Mwenyezi Mungu: Mjumbe alitumwa kwa mataifa kusema, “Jikusanyeni ili kuushambulia! Inukeni kwa ajili ya vita!”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 Nimesikia ujumbe kutoka kwa bwana: Mjumbe alitumwa kwa mataifa kusema, “Jikusanyeni ili kuushambulia! Inukeni kwa ajili ya vita!”

Tazama sura Nakili




Yeremia 49:14
12 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa maana wakuu wake wako Soani, na wajumbe wake wamefika Hanesi.


Tazama, nitatia roho ndani yake, naye atasikia uvumi, na kurudi hadi nchi yake mwenyewe, nami nitamwangusha kwa upanga katika nchi yake mwenyewe.


Maana nimekufanya mdogo kati ya mataifa, Na kudharauliwa katika watu.


Inoeni hiyo mishale; zishikeni ngao kwa nguvu; BWANA ameziamsha roho za wafalme wa Wamedi; kwa sababu shauri lake ni juu ya Babeli auangamize; maana ni kisasi cha BWANA, kisasi cha hekalu lake.


Wala isizimie mioyo yenu, wala msiiogope habari itakayosikiwa katika nchi; maana habari itakuja mwaka mmoja, na baadaye mwaka wa pili habari itakuja, na udhalimu katika nchi, mwenye kutawala akishindana na mwenye kutawala.


Nanyi mtasikia habari za vita na tetesi za vita; angalieni, msitishwe; maana hayo hayana budi kutukia; lakini ule mwisho bado.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo