Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 48:38 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

38 Juu ya madari yote ya nyumba za Moabu, na katika njia kuu zake, pana maombolezo, kila mahali; kwa maana nimevunja Moabu kama chombo kisichopendeza, asema BWANA.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

38 Juu ya nyumba za Moabu na katika viwanja vyao hakuna kinachosikika ila tu maombolezo. Mimi nimemvunja Moabu kama chombo kisichotakiwa na mtu. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

38 Juu ya nyumba za Moabu na katika viwanja vyao hakuna kinachosikika ila tu maombolezo. Mimi nimemvunja Moabu kama chombo kisichotakiwa na mtu. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

38 Juu ya nyumba za Moabu na katika viwanja vyao hakuna kinachosikika ila tu maombolezo. Mimi nimemvunja Moabu kama chombo kisichotakiwa na mtu. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

38 Juu ya mapaa yote katika Moabu na katika viwanja hakuna kitu isipokuwa maombolezo, kwa kuwa nimemvunja Moabu kama gudulia lisilotakiwa na mtu yeyote,” asema Mwenyezi Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

38 Juu ya mapaa yote katika Moabu na katika viwanja hakuna kitu chochote isipokuwa maombolezo, kwa kuwa nimemvunja Moabu kama gudulia ambalo hakuna mtu yeyote anayelitaka,” asema bwana.

Tazama sura Nakili




Yeremia 48:38
13 Marejeleo ya Msalaba  

Utawaponda kwa fimbo ya chuma, Na kuwavunja kama chombo cha mfinyanzi.


Wanajivika nguo za magunia katika njia kuu zao; juu ya madari yao, na katika mitaa yao, kila mtu analia, anamwaga machozi.


Ufunuo juu ya bonde la maono. Sasa una nini, wewe, Hata umepanda pia juu ya madari ya nyumba?


Naye atapavunja kama chombo cha mfinyanzi kivunjwavyo, kinavyovunjwavunjwa kikatili, hata hakipatikani katika vipande vyake kigae kitoshacho kutwaa moto jikoni, au kuteka maji kisimani.


Ndipo hapo utalivunja gudulia lile, mbele ya macho ya watu wale waendao pamoja nawe,


na kuwaambia, BWANA wa majeshi asema hivi, Hivyo ndivyo nitakavyowavunja watu hawa, na mji huu, kama mtu avunjavyo chombo cha mfinyanzi, kisichoweza kutengenezwa tena na kuwa kizima; nao watazika watu katika Tofethi hata pasibaki mahali pa kuzikia.


Je! Mtu huyu, Konia, ni chombo kilichodharauliwa, na kuvunjika? Ni chombo kisichopendeza? Mbona wametupwa, yeye na wazao wake, na kutupwa katika nchi wasiyoijua?


Ombolezeni, enyi wachungaji, na kulia; na kugaagaa katika majivu, enyi mlio hodari katika kundi; maana siku za kuuawa kwenu zimetimia kabisa, nami nitawavunja vipande vipande, nanyi mtaanguka kama chombo cha anasa.


Israeli amemezwa; sasa wamo miongoni mwa mataifa kama chombo kisichopendeza.


Niwaambialo ninyi katika giza, lisemeni katika nuru; na msikialo kwa siri, lihubirini juu ya nyumba.


naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, kama vyombo vya mfinyanzi vipondwavyo, kama mimi nami nilivyopokea kwa Baba yangu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo