Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 48:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

2 Sifa za Moabu haziko tena; katika Heshboni wameazimia mabaya juu yake, Haya! Njooni, na tumkatilie mbali asiwe taifa. Wewe nawe, Ee Madmena, utanyamazishwa; upanga utakufuatia.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 fahari ya Moabu imetoweka. Mpango ulifanywa huko Heshboni dhidi yake: ‘Haya! Tuwaangamize wasiwe tena taifa!’ Nawe Madmeni utanyamazishwa, upanga utakufuatia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 fahari ya Moabu imetoweka. Mpango ulifanywa huko Heshboni dhidi yake: ‘Haya! Tuwaangamize wasiwe tena taifa!’ Nawe Madmeni utanyamazishwa, upanga utakufuatia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 fahari ya Moabu imetoweka. Mpango ulifanywa huko Heshboni dhidi yake: ‘Haya! Tuwaangamize wasiwe tena taifa!’ Nawe Madmeni utanyamazishwa, upanga utakufuatia.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 Moabu haitasifiwa tena; huko Heshboni watu watapanga jinsi ya kumwangusha: ‘Njooni na tuliangamize taifa lile.’ Wewe nawe, ee Madmena, utanyamazishwa; upanga utakufuatia.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 Moabu haitasifiwa tena; huko Heshboni watu watafanya shauri baya la anguko lake: ‘Njooni na tuangamize taifa lile.’ Wewe nawe, ee Madmena, utanyamazishwa; upanga utakufuatia.

Tazama sura Nakili




Yeremia 48:2
20 Marejeleo ya Msalaba  

Ufunuo juu ya Moabu. Maana katika usiku mmoja Ari wa Moabu umeharibiwa kabisa na kuangamizwa; maana katika usiku mmoja Kiri wa Moabu umeharibiwa kabisa na kuangamizwa.


Moyo wangu unamlilia Moabu; wakuu wake wanakimbilia Soari kama ndama wa miaka mitatu; kwa maana wanapanda mbavu za Luhithi wakilia; maana katika njia iendayo hata Horonaimu wanatoa kilio cha maangamizi.


Lakini sasa BWANA asema hivi, Katika muda wa miaka mitatu, kama miaka ya mtu wa mshahara, utukufu wa Moabu utadharauliwa, licha ya wingi wa watu wake; na watakaobaki watakuwa wachache sana na dhaifu.


Kwa maana mkono wa BWANA utatulia katika mlima huu, na Moabu atakanyagwa chini huko aliko, kama vile majani makavu yakanyagwavyo katika maji machafu.


Maana BWANA, Mungu wa Israeli, aniambia hivi, Pokea kikombe cha divai ya ghadhabu hii mkononi mwangu, ukawanyweshe mataifa yote, ambao nitakupeleka kwao;


Ndipo nikakipokea kikombe kile mkononi mwa BWANA, nikawanywesha mataifa yote, ambao BWANA alinituma kwao;


Amri hizi zikiondoka, zisiwe mbele zangu, asema BWANA, ndipo wazao wa Israeli nao wataacha kuwa taifa mbele zangu milele.


Je! Hufikiri neno hili walilolisema watu hawa, wakinena, Jamaa zile mbili alizozichagua BWANA amezitupilia mbali? Hivyo ndivyo wanavyowadharau watu wangu, ili wasiwe taifa tena mbele yao.


Usiogope wewe, Ee Yakobo, mtumishi wangu, asema BWANA; kwa maana mimi ni pamoja nawe; maana nitawakomesha kabisa mataifa yote huko nilikokufukuza, bali sitakukomesha wewe kabisa; lakini nitakurudi kwa hukumu, wala sitakuacha bila adhabu.


Ninyi nyote mnaomzunguka, mlilieni, Nanyi nyote mlijuao jina lake, semeni, Jinsi ilivyovunjika fimbo ya enzi, Fimbo ile iliyokuwa nzuri!


Na Moabu ataangamizwa, asiwe taifa tena, kwa sababu alijitukuza juu ya BWANA.


Wamekimbia, wasio na nguvu Wanasimama chini ya kivuli cha Heshboni; Ila moto umetoka katika Heshboni, Na muali wa moto toka kati ya Sihoni Nao umekula pembe ya Moabu, Na utosi wa kichwa wa watu wapigao kelele.


Omboleza, Ee Heshboni, Kwa maana Ai umeangamizwa; Lieni, enyi binti za Raba, Mjivike nguo za magunia; Ombolezeni, mkipiga mbio Huko na huko kati ya maboma; Maana Malkamu atakwenda kuhamishwa, Makuhani wake na wakuu wake pamoja.


Nami nitawafadhaisha watu wa Elamu mbele ya adui zao, na mbele ya hao wanaowatafuta roho zao; nami nitawaletea mabaya, naam, hasira yangu kali, asema BWANA; nami nitautuma upanga uwafuatie, hadi nitakapowaangamiza;


Na wana wa Reubeni wakajenga Heshboni, na Eleale, na Kiriathaimu;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo