Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 46:23 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

23 Wataukata msitu wake, asema BWANA, ingawa haupenyeki; Kwa maana ni wengi kuliko nzige, hawahesabiki.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

23 Wataukata kabisa msitu wake, ingawa haupenyeki, nasema mimi Mwenyezi-Mungu, maana wao ni wengi kuliko nzige wasiohesabika.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

23 Wataukata kabisa msitu wake, ingawa haupenyeki, nasema mimi Mwenyezi-Mungu, maana wao ni wengi kuliko nzige wasiohesabika.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

23 Wataukata kabisa msitu wake, ingawa haupenyeki, nasema mimi Mwenyezi-Mungu, maana wao ni wengi kuliko nzige wasiohesabika.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

23 Wataufyeka msitu wake,” asema Mwenyezi Mungu, “hata kama umesongamana kiasi gani. Ni wengi kuliko nzige, hawawezi kuhesabika.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

23 Wataufyeka msitu wake,” asema bwana, “hata kama umesongamana kiasi gani. Ni wengi kuliko nzige, hawawezi kuhesabika.

Tazama sura Nakili




Yeremia 46:23
8 Marejeleo ya Msalaba  

Naye atauteketeza utukufu wa msitu wake, na wa shamba lake linalositawi, tangu nafsi hata nyama ya mwili, itakuwa kama vile afapo mtu aliye mgonjwa.


Nami nitawaadhibu kwa kadiri ya matendo yenu, asema BWANA; nami nitawasha moto katika msitu wake, nao utateketeza vitu vyote viuzungukavyo.


Sauti yake ni kama nyoka, wajapo kwa nguvu, Watamjia na mashoka, kama wachanja kuni.


Mwanadamu, uelekeze uso wako kusini, ukadondoze neno lako upande wa kusini, ukatabiri juu ya msitu wa uwanda wa Negebu,


Nami nitawarudishia hiyo miaka iliyoliwa na nzige, na parare, na madumadu, na tunutu, jeshi langu kubwa nililotuma kati yenu.


Kwa maana walikwea na ng'ombe zao na hema zao, wakaja mfano wa nzige kwa wingi; wao na ngamia zao pia walikuwa hawana hesabu; nao waliingia katika hiyo nchi ili kuiharibu.


Nao Wamidiani na Waamaleki na, hao wana wa mashariki walikuwa wametua bondeni, mfano wa nzige kwa wingi; na ngamia wao walikuwa hawana hesabu; mfano wa mchanga wa ufuoni, kwa wingi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo