Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 46:11 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

11 Panda uende Gileadi, ukatwae zeri, Ee binti, bikira wa Misri; unatumia dawa nyingi bure tu; hupati kupona kamwe.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Pandeni Gileadi, enyi watu wa Misri, mkachukue dawa ya marhamu. Mmetumia dawa nyingi bure; hakuna kitakachowaponya nyinyi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Pandeni Gileadi, enyi watu wa Misri, mkachukue dawa ya marhamu. Mmetumia dawa nyingi bure; hakuna kitakachowaponya nyinyi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Pandeni Gileadi, enyi watu wa Misri, mkachukue dawa ya marhamu. Mmetumia dawa nyingi bure; hakuna kitakachowaponya nyinyi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 “Panda hadi Gileadi ukapate zeri, ee Bikira Binti Misri. Lakini umetumia dawa nyingi bila mafanikio; huwezi kupona.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 “Panda hadi Gileadi ukapate zeri, ee Bikira Binti wa Misri. Lakini umetumia dawa nyingi bila mafanikio; huwezi kupona.

Tazama sura Nakili




Yeremia 46:11
15 Marejeleo ya Msalaba  

Nao wakakaa kitako kula chakula; wakainua macho yao, wakaona, msafara wa Waishmaeli wanakuja wakitoka Gileadi na ngamia zao, wakichukua ubani na zeri na manemane, wakisafiri kuvichukua mpaka Misri.


Israeli, baba yao, akawaambia, Kama ndivyo, fanyeni hivi; twaeni tunu za nchi katika vyombo vyenu, mkamchukulie mtu huyo zawadi, zeri kidogo, na asali kidogo, ubani, na manemane, na jozi, na lozi.


Haya, shuka, keti mavumbini, Ewe bikira, binti Babeli; Keti chini pasipo kiti cha enzi, Ewe binti wa Wakaldayo; Maana hutaitwa tena mwororo, mpenda anasa.


Nawe utawaambia neno hili, Macho yangu na yatiririke machozi, usiku na mchana, wala yasikome; kwa maana bikira, binti ya watu wangu, amevunjika mavunjiko makuu, kwa jeraha lisiloponyeka.


Jiwekee alama za njia; jifanyie miti ya kukuongoza; uuelekeze moyo wako kwenye njia kuu, njia ile ile uliyoiendea; rudi tena, Ee bikira wa Israeli, irudie hii miji yako.


Mara ya pili nitakujenga, nawe utajengwa, Ee bikira wa Israeli mara ya pili utapambwa kwa matari yako, nawe utatokea katika michezo yao wanaofurahi.


Babeli umeanguka na kuangamia ghafla; mwombolezeni; twaeni zeri kwa maumivu yake; ili labda apate kuponywa.


Je! Hakuna marhamu katika Gileadi? Huko hakuna tabibu? Mbona, basi, haijarejea afya ya binti ya watu wangu?


Yuda, na nchi ya Israeli, walikuwa wachuuzi wako; walitoa badala ya bidhaa yako ngano ya Minithi, na mtama, na asali, na mafuta, na zeri.


Kwa maana majeraha yake hayaponyeki; Maana msiba umeijia hata Yuda, Unalifikia lango la watu wangu, Naam, hata Yerusalemu.


Jeraha lako halipunguziki; donda lako haliponyeki; wote wasikiao habari zako wapiga makofi juu yako; kwa maana ni nani aliyewahi kuukwepa ukatili wako usio na mwisho?


Amin, nakuambia, Hutoki humo kamwe hadi utakapolipa senti ya mwisho.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo