Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 44:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

2 BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Ninyi mmeona mabaya yote niliyoleta juu ya Yerusalemu, na juu ya miji yote ya Yuda; na, tazama, ni ukiwa leo, wala hapana mtu akaaye ndani yake;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 “Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli asema hivi: Nyinyi mmeona maafa yote niliyouletea mji wa Yerusalemu na miji yote ya Yuda. Miji hii ni magofu mpaka leo wala hakuna mtu aishiye humo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 “Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli asema hivi: Nyinyi mmeona maafa yote niliyouletea mji wa Yerusalemu na miji yote ya Yuda. Miji hii ni magofu mpaka leo wala hakuna mtu aishiye humo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 “Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli asema hivi: Nyinyi mmeona maafa yote niliyouletea mji wa Yerusalemu na miji yote ya Yuda. Miji hii ni magofu mpaka leo wala hakuna mtu aishiye humo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 “Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, Mungu wa Israeli: Mliona maangamizi makubwa niliyoyaleta juu ya Yerusalemu na juu ya miji yote ya Yuda. Leo imeachwa ukiwa na magofu

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 “Hili ndilo asemalo bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli: Mliona maangamizi makubwa niliyoyaleta juu ya Yerusalemu na juu ya miji yote ya Yuda. Leo imeachwa ukiwa na magofu

Tazama sura Nakili




Yeremia 44:2
25 Marejeleo ya Msalaba  

Nami nitanyosha juu ya Yerusalemu kamba ya Samaria, na timazi ya nyumba ya Ahabu; nami nitaifuta Yerusalemu, kama mtu afutavyo sahani, kuifuta na kuifudikiza.


Mmeona jinsi nilivyowatendea Wamisri, na jinsi nilivyowachukua ninyi juu ya mbawa za tai, nikawaleta ninyi kwangu mimi.


Ndani ya mji umebaki ukiwa, na lango lake limepigwa kwa uharibifu.


Ndipo nilipouliza, Ee Bwana, hata lini? Naye akanijibu, Hadi miji itakapokuwa ukiwa, haina wenyeji, na nyumba zitakapokuwa hazina watu, na nchi hii itakapokuwa ganjo kabisa;


Na nchi hii yote pia itakuwa ukiwa, na kitu cha kushangaza; nayo mataifa haya yatamtumikia mfalme wa Babeli miaka sabini.


Tazama, nitawapa amri yangu, asema BWANA, na kuwarejesha kwenye mji huu; nao watapigana nao, na kuutwaa, na kuuteketeza kwa moto; nami nitaifanya miji ya Yuda kuwa ukiwa, isikaliwe na mtu.


Simba ametoka katika kichaka chake, ndiye aangamizaye mataifa; ameanza kushika njia, ametoka katika mahali pake; ili aifanye nchi yako kuwa ukiwa, miji yako ifanywe maganjo, asibaki mwenyeji ndani yake.


Hata BWANA asiweze kuvumilia tena, kwa sababu ya uovu wa matendo yenu, na kwa sababu ya machukizo mliyoyafanya; kwa sababu hiyo nchi yenu imekuwa ukiwa, na ajabu, na laana, isikaliwe na mtu kama ilivyo leo.


Kwa sababu mmefukiza uvumba, na kwa sababu mmetenda dhambi juu ya BWANA, wala hamkuitii sauti ya BWANA, wala hamkwenda katika torati yake, wala katika amri zake, wala katika shuhuda yake; ndiyo maana mabaya haya yamewapata kama ilivyo leo.


Ndipo katika miji ya Yuda, na katika njia kuu za Yerusalemu, nitaikomesha sauti ya kicheko na sauti ya furaha, sauti ya bwana arusi na sauti ya bibi arusi; kwa maana nchi hiyo itakuwa ukiwa.


Na kufa kutachaguliwa kuliko kuishi na mabaki wote waliosalia katika jamaa hii mbovu, waliosalia kila mahali nilikowafukuza, asema BWANA wa majeshi.


Nami nitafanya Yerusalemu kuwa magofu, Makao ya mbweha; Nami nitaifanya miji ya Yuda kuwa ukiwa, Isikaliwe na mtu awaye yote.


Jinsi mji huu ukaavyo ukiwa, Huo uliokuwa umejaa watu! Jinsi alivyokuwa kama mjane, Yeye aliyekuwa mkuu kati ya mataifa! Binti mfalme kati ya majimbo, Jinsi alivyoshikwa shokoa!


Mimi ninayalilia mambo hayo; Jicho langu, jicho langu linachuruzika machozi; Kwa kuwa mfariji yuko mbali nami, Ambaye ilimpasa kunihuisha nafsi; Watoto wangu wameachwa peke yao, Kwa sababu huyo adui ameshinda.


Kwa ajili ya mlima Sayuni ulio ukiwa, Mbweha hutembea juu yake.


Naye ameyathibitisha maneno yake, aliyoyanena juu yetu, na juu ya waamuzi wetu waliotuamua, kwa kumletea mambo maovu makuu; maana chini ya mbingu zote halikutendeka jambo kama hili, lilivyotendeka juu ya Yerusalemu.


Nami nitaifanya miji yenu iwe maganjo, na mahali penu patakatifu nitapatia ukiwa; wala sitasikia harufu ya manukato yenu yapendezayo.


Nchi nayo itaachwa na wao, nayo itazifurahia Sabato zake, itakapokuwa ukiwa pasipokuwa na wao; nao wataikubali adhabu ya uovu wao; kwa sababu wameyakataa maagizo yangu, na roho zao zimezichukia amri zangu.


Basi, kwa ajili yenu, Sayuni utalimwa kama shamba lilimwavyo, na Yerusalemu utakuwa magofu; na mlima wa nyumba utakuwa kama mahali palipoinuka msituni.


Lakini maneno yangu, na amri zangu nilizowaagiza hao manabii, watumishi wangu, je, Hazikuwapata baba zenu? Nao wakatubu na kusema, BWANA wa majeshi ametutenda kulingana na njia zetu, na matendo yetu, kama alivyokusudia kutenda.


Musa akawaita Israeli wote akawaambia, Mmeyaona yote BWANA aliyomfanya Farao katika nchi ya Misri mbele ya macho yenu, yeye na watumwa wake wote, na nchi yake yote;


nanyi mmeona mambo yote ambayo BWANA, Mungu wenu, amewatenda mataifa haya yote kwa ajili yenu; kwa maana BWANA, Mungu wenu, ndiye aliyewapigania ninyi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo