Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yeremia 43:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

4 Basi Yohana, mwana wa Karea, na wakuu wote wa majeshi, na watu wote hawakuitii sauti ya BWANA, kwamba wakae katika nchi ya Yuda.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Basi, Yohanani mwana wa Karea na makamanda wote wa majeshi pamoja na watu wote hawakutii aliyosema Mwenyezi-Mungu, kwamba wabaki katika nchi ya Yuda.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Basi, Yohanani mwana wa Karea na makamanda wote wa majeshi pamoja na watu wote hawakutii aliyosema Mwenyezi-Mungu, kwamba wabaki katika nchi ya Yuda.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Basi, Yohanani mwana wa Karea na makamanda wote wa majeshi pamoja na watu wote hawakutii aliyosema Mwenyezi-Mungu, kwamba wabaki katika nchi ya Yuda.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Basi Yohanani mwana wa Karea, na maafisa wote wa jeshi, na watu wote wakakataa kutii amri ya Mwenyezi Mungu ya kukaa katika nchi ya Yuda.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 Basi Yohanani mwana wa Karea, na maafisa wote wa jeshi, na watu wote wakakataa kutii amri ya bwana ya kukaa katika nchi ya Yuda.

Tazama sura Nakili




Yeremia 43:4
10 Marejeleo ya Msalaba  

Wakaondoka watu wote, wadogo kwa wakubwa, pamoja na wakuu wa majeshi, wakainuka kwenda Misri; kwa kuwa waliwaogopa Wakaldayo.


Ikawa, aliposema naye, mfalme akamwambia, Je! Tumekutia wewe kuwa mshauri wa mfalme? Nyamaza; kwa nini upigwe? Ndipo yule nabii akaacha, akasema, Najua ya kuwa Mungu amekusudia kukuangamiza, kwa sababu umeyafanya haya, wala hukulisikiliza shauri langu.


Umtumaini BWANA ukatende mema, Ukae katika nchi, upendezwe na uaminifu.


Ndipo niliposema, Bora hekima kuliko nguvu; lakini hekima ya maskini hudharauliwa, wala maneno yake hayasikilizwi.


Ndipo Yohana, mwana wa Karea, na viongozi wote wa majeshi waliokuwa pamoja naye, wakawatwaa hao watu wote waliosalia, aliowapata tena katika mikono ya Ishmaeli, mwana wa Nethania, huko Mizpa, baada ya kumwua Gedalia, mwana wa Ahikamu, yaani, watu wa vita, na wanawake na watoto, na matowashi, aliowarudisha toka Gibeoni;


nami nimewafunulia haya leo; lakini ninyi hamkuitii sauti ya BWANA, Mungu wenu, katika neno lolote ambalo amenituma kwenu.


Ndipo akamwita Yohana, mwana wa Karea, na makamanda wote wa majeshi waliokuwa pamoja naye, na watu wote tangu wadogo hata wakubwa,


Lakini hawakusikiliza, wala hawakutega masikio yao, ili wageuke na kuacha uovu wao, wasifukizie uvumba miungu mingine.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo