Yeremia 43:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC2 ndipo Azaria, mwana wa Hoshaya, na Yohana mwana wa Karea, na watu wote wenye kiburi wakanena, wakimwambia Yeremia, Unasema uongo; BWANA, Mungu wetu, hakukutuma useme, Msiende Misri kukaa huko; Tazama suraMatoleo zaidiBiblia Habari Njema2 Azaria mwana wa Hoshaia, Yohanani mwana wa Karea na watu wote mafidhuli, walimwambia Yeremia: “Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, hakukutuma wewe utuambie tusiende Misri, tukaishi huko. Tazama suraBiblia Habari Njema - BHND2 Azaria mwana wa Hoshaia, Yohanani mwana wa Karea na watu wote mafidhuli, walimwambia Yeremia: “Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, hakukutuma wewe utuambie tusiende Misri, tukaishi huko. Tazama suraBiblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza2 Azaria mwana wa Hoshaia, Yohanani mwana wa Karea na watu wote mafidhuli, walimwambia Yeremia: “Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, hakukutuma wewe utuambie tusiende Misri, tukaishi huko. Tazama suraNeno: Bibilia Takatifu2 Azaria mwana wa Hoshaya, na Yohanani mwana wa Karea, na watu wote wenye kiburi wakamwambia Yeremia, “Wewe unasema uongo! Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, hajakutuma kusema, ‘Kamwe msiende Misri kukaa huko.’ Tazama suraNeno: Maandiko Matakatifu2 Azaria mwana wa Hoshaya, na Yohanani mwana wa Karea, na watu wote wenye kiburi wakamwambia Yeremia, “Wewe unasema uongo! bwana Mwenyezi Mungu wetu hajakutuma kusema, ‘Kamwe msiende Misri kukaa huko.’ Tazama sura |
Ndipo Yohana, mwana wa Karea, na viongozi wote wa majeshi waliokuwa pamoja naye, wakawatwaa hao watu wote waliosalia, aliowapata tena katika mikono ya Ishmaeli, mwana wa Nethania, huko Mizpa, baada ya kumwua Gedalia, mwana wa Ahikamu, yaani, watu wa vita, na wanawake na watoto, na matowashi, aliowarudisha toka Gibeoni;