Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yeremia 43:10 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

10 ukawaambie, BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Tazama, nitatuma na kumtwaa Nebukadneza, mfalme wa Babeli, mtumishi wangu, nami nitaweka kiti chake cha enzi juu ya mawe haya niliyoyaficha; naye atatandaza hema yake ya fahari juu yake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

10 Kisha waambie hivi: Tazameni mimi nitamtuma na kumleta Nebukadneza, mfalme wa Babuloni, mtumishi wangu, naye ataweka kiti chake cha enzi juu ya mawe haya ambayo nimeyaficha hapa, na kutandaza paa la kifalme juu yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

10 Kisha waambie hivi: Tazameni mimi nitamtuma na kumleta Nebukadneza, mfalme wa Babuloni, mtumishi wangu, naye ataweka kiti chake cha enzi juu ya mawe haya ambayo nimeyaficha hapa, na kutandaza paa la kifalme juu yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

10 Kisha waambie hivi: Tazameni mimi nitamtuma na kumleta Nebukadneza, mfalme wa Babuloni, mtumishi wangu, naye ataweka kiti chake cha enzi juu ya mawe haya ambayo nimeyaficha hapa, na kutandaza paa la kifalme juu yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

10 Kisha uwaambie, ‘Hili ndilo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, Mungu wa Israeli, asemalo: Nitamtumania mtumishi wangu Nebukadneza mfalme wa Babeli, nami nitakiweka kiti chake cha utawala juu ya haya mawe niliyoyazika hapa, naye atatandaza hema lake la ufalme juu yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

10 Kisha uwaambie, ‘Hili ndilo bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo: Nitamtumania mtumishi wangu Nebukadneza mfalme wa Babeli, nami nitakiweka kiti chake cha enzi juu ya haya mawe niliyoyazika hapa, naye atatandaza hema yake ya ufalme juu yake.

Tazama sura Nakili




Yeremia 43:10
19 Marejeleo ya Msalaba  

Ikawa, Ben-hadadi alipolisikia neno hilo, naye alikuwa akinywa, yeye na wafalme, mabandani, aliwaambia watumwa wake, Jipangeni. Wakajipanga juu ya mji.


Wakatoka wakati wa adhuhuri. Lakini Ben-hadadi alikuwa akinywa hata kulewa mabandani, yeye na wale wafalme thelathini na wawili waliomsaidia.


Alifanya giza kuwa mahali pake pa kujificha, Kuwa hema yake ya kumzunguka. Akiwa katika giza la mawingu mazito yaliyojaa maji.


Maana atanisitiri bandani mwake siku ya mabaya, Atanisitiri katika sitara ya hema yake, Na kuniinua juu ya mwamba.


Utawasitiri kutoka kwa fitina za watu Katika maficho ya kuwapo kwako; Utawaficha katika hema Na ushindani wa ndimi.


nimwambiaye Koreshi, Mchungaji wangu, naye atayatenda mapenzi yangu; hata ataunena Yerusalemu, Utajengwa; na hilo hekalu, Msingi wako utawekwa.


Haya ndiyo BWANA amwambiayo Koreshi, masihi wake, ambaye nimemshika mkono wake wa kulia, ili kutiisha mataifa mbele yake, nami nitalegeza nguvu za wafalme; ili kufungua milango mbele yake, hata malango hayatafungwa.


Kwa kuwa, tazama, nitaziita jamaa zote za falme za kaskazini, asema BWANA; nao watakuja, na kuweka kila mtu kiti chake cha enzi mbele ya mahali pa kuingilia malango ya Yerusalemu, na kuzielekea kuta zake pande zote, na kuielekea miji yote ya Yuda.


Twaa mawe makubwa mikononi mwako, ukayafiche ndani ya chokaa ya kazi ya matofali, penye maingilio ya nyumba ya Farao huko Tapanesi, machoni pa watu wa Yuda;


Neno hili ndilo ambalo BWANA alimwambia Yeremia, nabii, kueleza jinsi Nebukadneza, mfalme wa Babeli, atakavyokuja na kuipiga nchi ya Misri.


nami nitaweka kiti changu cha enzi huko Elamu, nami nitawaharibu, mfalme na wakuu, watoke huko, asema BWANA.


Theluthi yenu mtakufa kwa tauni, na kwa njaa watakomeshwa ndani yako; na theluthi yenu wataanguka kwa upanga pande zako zote; na theluthi yenu nitawatawanya kwa pepo zote, kisha nitafuta upanga nyuma yao.


Yeye hubadili majira na nyakati; hutengua na kuteua wafalme; huwapa hekima wenye hekima; huwapa wenye ufahamu maarifa;


Basi yule mfalme akaghadhibika; akatuma majeshi yake, akawaangamiza wauaji wale, akauteketeza mji wao.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo