Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Yeremia 42:17 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

17 Haya ndiyo yatakayowapata watu wote waelekezao nyuso zao kwenda Misri, na kukaa huko; watakufa kwa upanga, na kwa njaa, na kwa tauni; hakuna mtu awaye yote miongoni mwao atakayesalia, au kuokoka katika mabaya nitakayoyaleta juu yao.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

17 Watu wote wenye nia ya kwenda kukaa Misri watakufa kwa njaa na maradhi mabaya wala hakuna hata mmoja wao atakayebaki au kunusurika kutokana na maafa nitakayowaletea.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

17 Watu wote wenye nia ya kwenda kukaa Misri watakufa kwa njaa na maradhi mabaya wala hakuna hata mmoja wao atakayebaki au kunusurika kutokana na maafa nitakayowaletea.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

17 Watu wote wenye nia ya kwenda kukaa Misri watakufa kwa njaa na maradhi mabaya wala hakuna hata mmoja wao atakayebaki au kunusurika kutokana na maafa nitakayowaletea.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

17 Naam, wote waliokusudia kwenda kuishi Misri watakufa kwa upanga, njaa na tauni; hakuna hata mmoja wao atakayenusurika au kuokoka maafa nitakayoyaleta juu yao.’

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

17 Naam, wote waliokusudia kwenda kuishi Misri watakufa kwa upanga, njaa na tauni; hakuna hata mmoja wao atakayenusurika au kuokoka maafa nitakayoyaleta juu yao.’

Tazama sura Nakili

Yeremia 42:17
7 Marejeleo ya Msalaba  

Nami nitatuma upanga, na njaa, na tauni, kati yao, hata watakapopotelea mbali katika nchi niliyowapa, wao na baba zao.

BWANA asema hivi, Akaaye ndani ya mji huu atakufa kwa upanga, na kwa njaa, na kwa tauni; bali yeye atokaye kwenda kwa Wakaldayo ataishi, naye atapewa maisha yake yawe kama nyara, naye ataishi.

basi, lisikieni neno la BWANA, enyi mabaki ya Yuda; BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Ikiwa mnakaza nyuso zenu kuingia Misri, na kwenda kukaa huko;

Basi, sasa jueni sana ya kuwa mtakufa kwa upanga, na kwa njaa, na kwa tauni, katika mahali pale mnapopatamani kwenda na kukaa.

Nao watakaoukimbia upanga, watatoka katika nchi ya Misri, na kuiingia katika nchi ya Yuda, watu wachache sana; na wote wa Yuda waliosalia, waliokwenda katika nchi ya Misri ili kukaa huko, watajua ni neno la nani litakalosimama, neno langu, au neno lao.

Ninyi mmeuogopa upanga; nami nitauleta upanga juu yenu, asema Bwana MUNGU.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo