Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yeremia 42:11 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

11 Msimwogope mfalme wa Babeli, mnayemwogopa; msimwogope, asema BWANA; maana mimi ni pamoja nanyi, niwaokoe, na kuwaponya kutoka kwa mkono wake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Msimwogope mfalme wa Babuloni mnayemwogopa; naam, msimwogope hata kidogo. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema. Mimi niko pamoja nanyi kuwaokoeni na kuwasalimisha kutoka mikononi mwake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Msimwogope mfalme wa Babuloni mnayemwogopa; naam, msimwogope hata kidogo. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema. Mimi niko pamoja nanyi kuwaokoeni na kuwasalimisha kutoka mikononi mwake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Msimwogope mfalme wa Babuloni mnayemwogopa; naam, msimwogope hata kidogo. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema. Mimi niko pamoja nanyi kuwaokoeni na kuwasalimisha kutoka mikononi mwake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Msimwogope mfalme wa Babeli, ambaye sasa mnamwogopa. Msimwogope, asema Mwenyezi Mungu, kwa kuwa niko pamoja nanyi, nami nitawaokoa na kuwaponya kutoka mkononi mwake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 Msimwogope mfalme wa Babeli, ambaye sasa mnamwogopa. Msimwogope, asema bwana, kwa kuwa niko pamoja nanyi, nami nitawaokoa na kuwaponya kutoka mikononi mwake.

Tazama sura Nakili




Yeremia 42:11
25 Marejeleo ya Msalaba  

Wakaondoka watu wote, wadogo kwa wakubwa, pamoja na wakuu wa majeshi, wakainuka kwenda Misri; kwa kuwa waliwaogopa Wakaldayo.


BWANA yuko upande wangu, sitaogopa; Mwanadamu atanitenda nini?


BWANA wa majeshi yu pamoja nasi, Mungu wa Yakobo ni kimbilio letu.


BWANA wa majeshi yu pamoja nasi, Mungu wa Yakobo ni ngome yetu.


usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kulia wa haki yangu.


Upitapo katika maji mengi nitakuwa pamoja nawe; na katika mito, haitakugharikisha; uendapo katika moto, hutateketea; wala mwali wa moto hautakuunguza.


Usiogope; maana mimi ni pamoja nawe; nitaleta wazao wako toka mashariki, nitakukusanya toka magharibi;


Nao watapigana nawe; lakini hawatakushinda; maana mimi nipo pamoja nawe, asema BWANA, ili nikuokoe.


Usiogope kwa sababu ya hao maana mimi nipo pamoja nawe nikuokoe, asema BWANA.


Nami nitakufanya kuwa kama ukuta wa boma la shaba juu ya watu hawa; nao watapigana nawe; lakini hawatakushinda; maana mimi nipo pamoja nawe, ili nikuokoe, na kukuponya, asema BWANA.


Bali taifa lile watakaotia shingo zao katika nira ya mfalme wa Babeli, na kumtumikia, taifa hilo nitawaacha wakae katika nchi yao wenyewe, asema BWANA; nao watailima, na kukaa ndani yake.


Nikamwambia Sedekia, mfalme wa Yuda, kwa mfano wa maneno hayo yote, nikisema, Tieni shingo zenu katika nira ya mfalme wa Babeli, mkamtumikie yeye na watu wake, mpate kuishi.


Msiwasikilize; mtumikieni mfalme wa Babeli, mkaishi; kwa nini mji huu ufanywe kuwa ukiwa?


kwa sababu ya Wakaldayo; maana waliwaogopa, kwa sababu Ishmaeli, mwana wa Nethania, amemwua Gedalia, mwana wa Ahikamu, ambaye mfalme wa Babeli amemweka kuwa mtawala juu ya nchi.


Lakini msimwasi BWANA, wala msiwaogope wale wenyeji wa nchi, maana wao ni chakula kwetu; kinga iliyokuwa juu yao imeondolewa, naye BWANA yuko pamoja nasi; msiwaogope.


Msiwaogope wauuao mwili, wasiweze kuiua na roho; afadhali mwogopeni yule awezaye kuangamiza mwili na roho pia katika Jehanamu.


na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.


kwa kuwa mimi ni pamoja nawe, wala hapana mtu atakayekushambulia ili kukudhuru; kwa maana mimi nina watu wengi katika mji huu.


Basi, tuseme nini juu ya hayo? Mungu akiwapo upande wetu, ni nani awezaye kutupinga?


kwa maana BWANA, Mungu wenu, ndiye awaandamaye kwenda kuwapigania juu ya adui zenu, ili kuwaokoa ninyi.


Lakini Bwana alisimama pamoja nami akanitia nguvu, ili kwa kazi yangu ule ujumbe utangazwe kwa utimilifu, hata wasikie Mataifa yote; nami nikaokolewa kutoka kwa kinywa cha simba.


Hakuna mtu yeyote atakayeweza kusimama mbele yako siku zote za maisha yako; kama nilivyokuwa pamoja na Musa, ndivyo nitakavyokuwa pamoja na wewe; sitakupungukia wala sitakuacha.


Je! Si mimi niliyekuamuru? Uwe hodari na moyo wa ushujaa; usiogope wala usifadhaike; kwa kuwa BWANA, Mungu wako, yu pamoja nawe kila uendako.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo