Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yeremia 41:18 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

18 kwa sababu ya Wakaldayo; maana waliwaogopa, kwa sababu Ishmaeli, mwana wa Nethania, amemwua Gedalia, mwana wa Ahikamu, ambaye mfalme wa Babeli amemweka kuwa mtawala juu ya nchi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

18 walikuwa wanawaogopa Wakaldayo tangu wakati Ishmaeli mwana wa Nethania, alipomuua Gedalia mwana wa Ahikamu ambaye mfalme wa Babuloni alikuwa amemteua kuwa mtawala wa nchi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

18 walikuwa wanawaogopa Wakaldayo tangu wakati Ishmaeli mwana wa Nethania, alipomuua Gedalia mwana wa Ahikamu ambaye mfalme wa Babuloni alikuwa amemteua kuwa mtawala wa nchi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

18 walikuwa wanawaogopa Wakaldayo tangu wakati Ishmaeli mwana wa Nethania, alipomuua Gedalia mwana wa Ahikamu ambaye mfalme wa Babuloni alikuwa amemteua kuwa mtawala wa nchi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

18 ili kuwatoroka Wakaldayo. Waliwaogopa kwa sababu Ishmaeli mwana wa Nethania alikuwa amemuua Gedalia mwana wa Ahikamu, aliyekuwa amewekwa na mfalme wa Babeli kuwa mtawala wa nchi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

18 ili kuwatoroka Wakaldayo. Waliwaogopa kwa sababu Ishmaeli mwana wa Nethania alikuwa amemuua Gedalia mwana wa Ahikamu, ambaye alikuwa amewekwa na mfalme wa Babeli kuwa mtawala wa nchi.

Tazama sura Nakili




Yeremia 41:18
11 Marejeleo ya Msalaba  

Na kwa habari ya watu waliosalia katika nchi ya Yuda, aliowasaza Nebukadneza, mfalme wa Babeli, akamweka Gedalia mwana wa Ahikamu mwana wa Shafani awe mtawala juu yao.


Lakini ikawa katika mwezi wa saba Ishmaeli mwana wa Nethania, mwana wa Elishama, mmoja wa wazao wa kifalme, na watu kumi pamoja naye, wakamwendea Gedalia, wakampiga hata akafa, na hao Wayahudi na Wakaldayo waliokuwa pamoja naye huko Mispa.


Tena ni nani uliyemwogopa na kumhofu, hata ukasema uongo, wala hukunikumbuka mimi, wala kuweka hayo moyoni? Je! Mimi sikunyamaza tangu zamani, hata huniogopi?


Alipokuwa bado hajaenda, akasema, Rudi sasa kwa Gedalia, mwana wa Ahikamu, mwana wa Shafani, ambaye mfalme wa Babeli amemweka kuwa mtawala juu ya miji ya Yuda, ukakae pamoja naye kati ya watu; au nenda popote utakapoona mwenyewe kuwa pakufaa. Basi, mkuu wa askari walinzi akampa vyakula na zawadi, akamwacha aende zake.


Ndipo makamanda, wote wa majeshi, na Yohana, mwana wa Karea, na Yezania, mwana wa Hoshaya, na watu wote tangu wadogo hata wakubwa, wakakaribia,


Msimwogope mfalme wa Babeli, mnayemwogopa; msimwogope, asema BWANA; maana mimi ni pamoja nanyi, niwaokoe, na kuwaponya kutoka kwa mkono wake.


basi, itakuwa, upanga mnaouogopa utawapata huko, katika nchi ya Misri, nayo njaa mnayoiogopa itawafuatia mbio huko Misri, nanyi mtakufa huko.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo