Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yeremia 4:17 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

17 Kama watu walindao shamba, wameuzunguka wauhusuru; kwa sababu ameniasi mimi, asema BWANA.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

17 wanauzingira Yerusalemu kama walinda mashamba, kwa sababu watu wake wameniasi mimi Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

17 wanauzingira Yerusalemu kama walinda mashamba, kwa sababu watu wake wameniasi mimi Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

17 wanauzingira Yerusalemu kama walinda mashamba, kwa sababu watu wake wameniasi mimi Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

17 Wamemzunguka kama watu walindao shamba, kwa sababu amefanya uasi dhidi yangu,’ ” asema Mwenyezi Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

17 Wamemzunguka kama watu walindao shamba, kwa sababu amefanya uasi dhidi yangu,’ ” asema bwana.

Tazama sura Nakili




Yeremia 4:17
16 Marejeleo ya Msalaba  

Walakini hawakukutii, wakakuasi, wakaitupa sheria yako nyuma yao, wakawaua manabii wako waliowaonya ili wapate kukurudia wewe; wakakufuru sana.


Lakini miaka mingi ukachukuliana nao, nawe ukawashuhudia kwa roho yako kwa vinywa vya manabii wako; wao wasitake kusikiliza; kwa hiyo ukawatia katika mikono ya watu wa nchi.


Na binti Sayuni ameachwa kama kibanda katika shamba la mizabibu, kama kipenu katika shamba la matango, kama mji uliohusuriwa.


Kwa maana watu hawa ni watu waasi, watoto wasemao uongo, watoto wasiotaka kuisikia sheria ya BWANA;


Lakini watu hawa wana moyo wa kuasi na ukaidi; wameasi, wamekwenda zao.


Ikawa, katika mwaka wa tisa wa kumiliki kwake, katika mwezi wa kumi, na siku ya kumi ya mwezi huo, Nebukadneza, mfalme wa Babeli, akaja, yeye na jeshi lake lote, juu ya Yerusalemu, akapanga hema zake juu yake; nao wakajenga ngome juu yake pande zote.


BWANA ndiye mwenye haki; Maana nimeiasi amri yake; Sikieni, nawasihi, enyi watu wote, Mkayatazame majonzi yangu; Wasichana wangu na wavulana wangu Wamechukuliwa mateka.


Yerusalemu amefanya dhambi sana; Kwa hiyo amekuwa kama kitu kichafu; Wote waliomheshimu wanamdharau, Kwa sababu wameuona uchi wake; Naam, yeye anaugua, Na kujigeuza aende nyuma.


Mmekuwa na uasi juu ya BWANA tokea siku nilipowajua ninyi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo