Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yeremia 39:9 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

9 Basi, Nebuzaradani, mkuu wa askari walinzi, akawachukua mateka mabaki ya watu waliosalia katika mji mpaka Babeli, na hao pia waliouacha mji na kujiunga naye, na mabaki ya watu waliosalia.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 Kisha, Nebuzaradani, kapteni wa walinzi wa mfalme, aliwapeleka uhamishoni Babuloni watu waliokuwa wamebaki mjini na wale waliokuwa wamejisalimisha kwake pamoja na watu wote waliokuwa wamebaki.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 Kisha, Nebuzaradani, kapteni wa walinzi wa mfalme, aliwapeleka uhamishoni Babuloni watu waliokuwa wamebaki mjini na wale waliokuwa wamejisalimisha kwake pamoja na watu wote waliokuwa wamebaki.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 Kisha, Nebuzaradani, kapteni wa walinzi wa mfalme, aliwapeleka uhamishoni Babuloni watu waliokuwa wamebaki mjini na wale waliokuwa wamejisalimisha kwake pamoja na watu wote waliokuwa wamebaki.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 Nebuzaradani mkuu wa askari walinzi wa mfalme akawachukua na kuwapeleka uhamishoni Babeli watu waliokuwa wamebaki ndani ya mji, pamoja na wale waliokuwa wamejisalimisha kwake, na watu wengine wote.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 Nebuzaradani kiongozi wa walinzi wa mfalme akawachukua na kuwapeleka uhamishoni Babeli watu waliokuwa wamebaki ndani ya mji, pamoja na wale waliokuwa wamejisalimisha kwake, na watu wengine wote.

Tazama sura Nakili




Yeremia 39:9
20 Marejeleo ya Msalaba  

Nao Wamidiani wakamuuza huko Misri, kwa Potifa, mmoja wa maofisa wa Farao, mkuu wa askari walinzi.


Na baadhi ya wanao watakaotoka kwako, utakaowazaa, watawachukulia mbali; nao watakuwa matowashi jumbani mwake mfalme wa Babeli.


Na mabaki ya watu waliosalia katika mji, nao wale walioasi, na kumkimbilia mfalme wa Babeli, na mabaki ya watu wote wengine, watu hao Nebuzaradani, kamanda wa askari walinzi, akawachukua mateka.


Kisha Nebuzaradani, kamanda wa askari walinzi, akawatwaa hao, akawaleta kwa mfalme wa Babeli huko Ribla.


Kwa sababu hiyo watu wangu wamechukuliwa mateka, kwa kukosa kuwa na maarifa; na watu wao wenye cheo wana njaa, na wengi wao waona kiu sana.


Maana BWANA asema hivi, Tazama, wakati huu nitawatupa wenyeji wa nchi hii kama kwa kombeo, nitawataabisha, wapate kuona taabu.


basi, kwa sababu hiyo, nitawatoeni katika nchi hii, na kuwaingiza katika nchi ambayo hamkuijua, wala ninyi wala baba zenu; na huko mtawatumikia miungu mingine mchana na usiku; kwa maana mimi sitawapa fadhili zangu hata kidogo.


Na habari za tini zile mbovu, zisizoweza kuliwa, kwa kuwa ni mbovu sana; hakika, asema, BWANA, ndivyo nitakavyomtoa Sedekia, mfalme wa Yuda, na wakuu wake, na mabaki ya Yerusalemu, waliosalia katika nchi hii, na hao wanaokaa katika nchi ya Misri.


Mfalme Sedekia akamwambia Yeremia, Nawaogopa Wayahudi waliowakimbilia Wakaldayo, wasije wakanitia katika mikono yao, nao wakanidhihaki.


Neno hili ndilo lililomjia Yeremia, kutoka kwa BWANA, baada ya wakati ule Nebuzaradani, mkuu wa askari walinzi, alipomwacha aende zake toka Rama, baada ya kumchukua akiwa amefungwa minyororo, pamoja na wafungwa wote wa Yerusalemu na Yuda, waliochukuliwa wakiwa wamefungwa mpaka Babeli.


Kisha, wakuu wote wa majeshi waliokuwa katika bara, wao na watu wao, waliposikia kwamba mfalme wa Babeli amemweka Gedalia, mwana wa Ahikamu, kuwa mtawala juu ya nchi, na kwamba amemkabidhi wanaume na wanawake na watoto, na baadhi ya maskini wa nchi wasiochukuliwa mateka Babeli;


Na Nebuzaradani, mkuu wa askari walinzi, akawatwaa, akawaleta kwa mfalme wa Babeli huko Ribla.


Naye mfalme wa Babeli akawapiga na kuwaua huko Ribla katika nchi ya Hamathi. Ndivyo Yuda alivyochukuliwa utumwani, akatolewa katika nchi yake.


Ndipo Danieli kwa busara na hadhari akamjibu Arioko, mkuu wa walinzi wa mfalme, aliyekuwa ametoka ili kuwaua wenye hekima wa Babeli;


Nanyi nitawatapanyatapanya katika mataifa, nami nitaufuta upanga nyuma yenu; na nchi yenu itakuwa ni ukiwa, na miji yenu maganjo.


Na BWANA atawatawanya kati ya mataifa, nanyi mtasalia watu wachache kati ya makabila, mtakakopelekwa mbali na BWANA.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo