Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 39:17 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

17 Lakini nitakuokoa wewe katika siku hiyo, asema BWANA; wala hutatiwa katika mikono ya watu wale unaowaogopa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

17 Lakini siku hiyo mimi nitakuokoa wewe, wala hutatiwa mikononi mwa watu unaowaogopa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

17 Lakini siku hiyo mimi nitakuokoa wewe, wala hutatiwa mikononi mwa watu unaowaogopa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

17 Lakini siku hiyo mimi nitakuokoa wewe, wala hutatiwa mikononi mwa watu unaowaogopa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

17 Lakini siku hiyo nitakuokoa, asema Mwenyezi Mungu; hutatiwa mikononi mwa wale unaowaogopa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

17 Lakini siku hiyo nitakuokoa, asema bwana; hutatiwa mikononi mwa wale unaowaogopa.

Tazama sura Nakili




Yeremia 39:17
16 Marejeleo ya Msalaba  

Baada ya mambo hayo neno la BWANA likamjia Abramu katika njozi, likinena, Usiogope, Abramu, Mimi ni ngao yako, na thawabu yako itakuwa kubwa sana.


Naye Daudi akamwambia Gadi, Nimeingia katika mashaka sana; basi sasa na tuanguke katika mkono wa BWANA; kwa kuwa rehema zake ni nyingi; wala nisianguke katika mkono wa wanadamu.


Eliya akasema, Kama BWANA wa majeshi aishivyo ambaye ninasimama mbele zake, hakika nitajionesha kwake leo.


Basi, Obadia akaenda zake amwone Ahabu, akamwambia; naye Ahabu akaenda kumlaki Eliya.


Akamjibu, Usiogope; maana walio pamoja nasi ni wengi kuliko wale walio pamoja nao.


Uniite siku ya mateso; Nitakuokoa, nawe utanitukuza.


Nao watapigana nawe; lakini hawatakushinda; maana mimi nipo pamoja nawe, asema BWANA, ili nikuokoe.


Na Shefatia, mwana wa Matani, na Gedalia, mwana wa Pashuri, na Yukali, mwana wa Shelemia, na Pashuri, mwana wa Malkiya, wakayasikia maneno ambayo Yeremia aliwaambia watu wote, akisema,


Ee bwana wangu, mfalme, watu hawa wametenda mabaya katika mambo yote waliyomtenda Yeremia, nabii, ambaye wamemtupa shimoni; naye hakosi atakufa pale alipo, kwa sababu ya njaa; kwa kuwa hakuna mkate kabisa katika mji.


Basi mfalme akatoa amri, nao wakamleta Danieli, wakamtupa katika tundu la simba. Mfalme akanena, akamwambia Danieli, Mungu wako unayemtumikia daima, yeye atakuponya.


Na Mfalme atajibu, akiwaambia, Amin, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo