Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yeremia 39:11 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

11 Basi Nebukadneza, mfalme wa Babeli, akamwagiza Nebuzaradani, mkuu wa askari walinzi, katika habari za Yeremia, akisema,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Nebukadneza mfalme wa Babuloni alikuwa amempa Nebuzaradani kapteni wa walinzi, amri ifuatayo kuhusu Yeremia:

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Nebukadneza mfalme wa Babuloni alikuwa amempa Nebuzaradani kapteni wa walinzi, amri ifuatayo kuhusu Yeremia:

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Nebukadneza mfalme wa Babuloni alikuwa amempa Nebuzaradani kapteni wa walinzi, amri ifuatayo kuhusu Yeremia:

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Basi, Nebukadneza mfalme wa Babeli alikuwa ametoa maagizo kuhusu Yeremia kupitia Nebuzaradani mkuu wa askari walinzi wa mfalme akisema:

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 Basi, Nebukadneza mfalme wa Babeli alikuwa ametoa maagizo kuhusu Yeremia kupitia Nebuzaradani kiongozi wa walinzi wa mfalme akisema:

Tazama sura Nakili




Yeremia 39:11
12 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini yeye huokoa na upanga wa kinywa chao, Hata kumwokoa mhitaji na mkono wake aliye hodari.


Basi hivi huyo maskini ana matumaini, Na uovu hufumba kinywa chake.


Yeye atakuokoa na mateso sita; Naam, hata katika saba hapana uovu utakaokugusa.


Usiogope kwa sababu ya hao maana mimi nipo pamoja nawe nikuokoe, asema BWANA.


BWANA akasema, Hakika nitakutia nguvu upate mema; hakika nitamlazimisha adui akusihi wakati wa uovu, na wakati wa taabu.


Nami nitakufanya kuwa kama ukuta wa boma la shaba juu ya watu hawa; nao watapigana nawe; lakini hawatakushinda; maana mimi nipo pamoja nawe, ili nikuokoe, na kukuponya, asema BWANA.


Nami nitakuokoa kutoka kwa mkono wa watu wabaya, nami nitakukomboa kutoka kwa mkono wao wenye kutisha.


Lakini yeye, wala watumishi wake, wala watu wa nchi, hawakuyasikiliza maneno ya BWANA aliyonena kwa kinywa cha nabii Yeremia.


Neno hili ndilo lililomjia Yeremia, kutoka kwa BWANA, baada ya wakati ule Nebuzaradani, mkuu wa askari walinzi, alipomwacha aende zake toka Rama, baada ya kumchukua akiwa amefungwa minyororo, pamoja na wafungwa wote wa Yerusalemu na Yuda, waliochukuliwa wakiwa wamefungwa mpaka Babeli.


Na sasa, tazama, nakufungulia leo minyororo hii iliyo mikononi mwako. Kama ukiona ni vema kwenda Babeli pamoja nami, haya! Njoo, nami nitakutunza sana; lakini kama ukiona ni vibaya kwenda Babeli pamoja nami, basi, acha; tazama, nchi yote iko mbele yako; palipo pema machoni pako na pa kukufaa, nenda huko.


Basi katika mwezi wa tano, siku ya kumi ya mwezi, ndio mwaka wa kumi na tisa wa mfalme Nebukadneza, mfalme wa Babeli; Nebuzaradani, kamanda wa askari walinzi, aliyesimama mbele ya mfalme wa Babeli, aliingia Yerusalemu.


Akamwamuru yule ofisa kwamba Paulo alindwe; ila awe na nafasi, wala asimkataze mmojawapo wa rafiki zake kumtumikia.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo