Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yeremia 39:10 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

10 Lakini Nebuzaradani, kamanda wa askari walinzi, akawaacha baadhi ya maskini wa watu, waliokuwa hawana kitu, katika nchi ya Yuda, akawapa mashamba ya mizabibu na mashamba wakati uo huo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

10 Nebuzaradani, kapteni wa walinzi wa mfalme, aliwaacha katika nchi ya Yuda baadhi ya watu maskini ambao hawakuwa na chochote, akawagawia mashamba ya mizabibu na kuwapa maeneo ya kulima wakati huohuo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

10 Nebuzaradani, kapteni wa walinzi wa mfalme, aliwaacha katika nchi ya Yuda baadhi ya watu maskini ambao hawakuwa na chochote, akawagawia mashamba ya mizabibu na kuwapa maeneo ya kulima wakati huohuo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

10 Nebuzaradani, kapteni wa walinzi wa mfalme, aliwaacha katika nchi ya Yuda baadhi ya watu maskini ambao hawakuwa na chochote, akawagawia mashamba ya mizabibu na kuwapa maeneo ya kulima wakati huohuo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

10 Lakini Nebuzaradani mkuu wa askari walinzi aliwabakiza baadhi ya watu maskini katika nchi ya Yuda, ambao hawakuwa na kitu. Naye wakati huo akawapa mashamba ya mizabibu na mashamba mengine.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

10 Lakini Nebuzaradani kiongozi wa walinzi aliwabakiza baadhi ya watu maskini katika nchi ya Yuda, ambao hawakuwa na kitu. Naye wakati huo akawapa mashamba ya mizabibu na mashamba mengine.

Tazama sura Nakili




Yeremia 39:10
8 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini huyo kamanda wa askari walinzi akawaacha watu walio maskini ili wawe watunza mizabibu na wakulima.


Katika siku hiyo itakuwa ya kwamba mtu atalisha ng'ombe jike mchanga na kondoo wawili wa kike;


Na mimi, tazama, nitakaa Mizpa, ili nisimame mbele ya Wakaldayo watakaotujia; lakini ninyi chumeni divai, na matunda ya wakati wa jua, na mafuta, mkaviweke vitu hivyo katika vyombo vyenu, mkakae katika miji yenu mliyoitwaa.


Kisha, wakuu wote wa majeshi waliokuwa katika bara, wao na watu wao, waliposikia kwamba mfalme wa Babeli amemweka Gedalia, mwana wa Ahikamu, kuwa mtawala juu ya nchi, na kwamba amemkabidhi wanaume na wanawake na watoto, na baadhi ya maskini wa nchi wasiochukuliwa mateka Babeli;


wanaume, na wanawake, na watoto, na binti za mfalme, na kila mtu ambaye Nebuzaradani, mkuu wa askari walinzi, amemwacha pamoja na Gedalia, mwana wa Ahikamu, mwana wa Shafani, pia na Yeremia, nabii, na Baruku, mwana wa Neria;


Lakini Nebuzaradani, kamanda wa askari walinzi, akawaacha watu walio maskini kabisa ili wawe watunza mizabibu na wakulima.


Mwanadamu, watu wale wakaao mahali palipoharibika katika nchi ya Israeli husema ya kwamba, Abrahamu alikuwa mmoja, akairithi nchi hii; lakini sisi tu watu wengi; tumepewa nchi hii iwe urithi wetu.


Basi nikalilisha kundi la machinjo, kweli kondoo waliokuwa wanyonge kabisa. Kisha nikajipatia fimbo mbili; nami nikaiita ya kwanza, Neema, na ya pili nikaiita, Umoja; nikalilisha kundi lile.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo