Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yeremia 34:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

5 utakufa katika amani; na kama walivyofukizia baba zako, wafalme wa zamani waliokutangulia, ndivyo watakavyokufukizia; na kukulilia wakisema, Aa, BWANA! Kwa maana mimi nimelinena neno hili, asema BWANA.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 Utakufa kwa amani. Na, kama vile watu walivyochoma ubani walipowazika wazee wako waliokuwa wafalme, ndivyo watakavyokuchomea ubani na kuomboleza wakisema, ‘Maskini! Mfalme wetu amefariki!’ Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 Utakufa kwa amani. Na, kama vile watu walivyochoma ubani walipowazika wazee wako waliokuwa wafalme, ndivyo watakavyokuchomea ubani na kuomboleza wakisema, ‘Maskini! Mfalme wetu amefariki!’ Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 Utakufa kwa amani. Na, kama vile watu walivyochoma ubani walipowazika wazee wako waliokuwa wafalme, ndivyo watakavyokuchomea ubani na kuomboleza wakisema, ‘Maskini! Mfalme wetu amefariki!’ Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 bali utakufa kwa amani. Kama vile watu walivyowasha moto wa maziko kwa heshima ya baba zako, wafalme waliokutangulia, ndivyo watu watakavyowasha moto kwa heshima yako na kuomboleza, wakisema: “Ole, Ee Mwenyezi Mungu!” Mimi mwenyewe ninaweka ahadi hii, asema Mwenyezi Mungu.’ ”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 utakufa kwa amani. Kama vile watu walivyowasha moto wa maziko kwa heshima ya baba zako, wafalme waliokutangulia, ndivyo watu watakavyowasha moto kwa heshima yako na kuomboleza, wakisema: “Ole, Ee bwana!” Mimi mwenyewe ninaweka ahadi hii, asema bwana.’ ”

Tazama sura Nakili




Yeremia 34:5
10 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa hiyo tazama, nitakukusanya pamoja na baba zako, nawe utawekwa kaburini mwako kwa amani; wala macho yako hayatauona uovu huo wote nitakaouleta juu ya mahali hapa. Basi wakamletea mfalme habari tena.


Wakamzika katika makaburi yake mwenyewe, aliyojichimbia katika mji wa Daudi, wakamlaza juu ya kitanda kilichojazwa manukato, na kila namna ya machanganyiko ya hao mafundi wa dawa; wakawasha moto mkubwa sana kwa heshima yake.


Tazama, nitakukusanya kwa baba zako, nawe utawekwa kaburini mwako kwa amani, wala macho yako hayataona mabaya yote nitakayoyaleta juu ya mahali hapa, na juu ya wakaao. Basi wakamrudishia mfalme habari.


Basi, BWANA asema hivi, kuhusu habari za Yehoyakimu, mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda; Hawatamwombolezea, wakisema, Aa! Ndugu yangu; au, Aa! Dada yangu; wala hawatamlilia, wakisema, Aa! Bwana wangu; au, Aa! Utukufu wake.


Hata hivyo lisikie neno la BWANA, Ee Sedekia, mfalme wa Yuda; BWANA asema hivi kukuhusu; hutakufa kwa upanga;


Pumzi ya mianzi ya pua zetu, masihi wa BWANA, Alikamatwa katika marima yao; Ambaye kwa habari zake tulisema, Chini ya kivuli chake tutakaa kati ya mataifa.


Kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, hakika mahali pale akaapo mfalme aliyemweka awe mfalme, ambaye alikidharau kiapo chake, na kulivunja agano lake, ndipo atakapokufa pamoja naye kati ya Babeli.


Ndipo Nebukadneza, mfalme, akaanguka kifudifudi, akamsujudia Danieli, akatoa amri wamtolee Danieli sadaka na uvumba.


wakainuka mashujaa wote, wakaenda usiku kucha, wakautwaa mwili wake Sauli, na miili ya wanawe, na kuiondoa ukutani kwa Beth-sheani nao wakaja Yabeshi, na kuiteketeza huko.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo