Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 33:15 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

15 Katika siku zile, na wakati ule, nitamchipushia Daudi Chipukizi la haki; naye atafanya hukumu na haki katika nchi hii.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 Katika siku hizo, naam, wakati huo, nitachipusha chipukizi mwadilifu wa uzao wa Daudi. Chipukizi huyo atatekeleza haki na uadilifu katika nchi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 Katika siku hizo, naam, wakati huo, nitachipusha chipukizi mwadilifu wa uzao wa Daudi. Chipukizi huyo atatekeleza haki na uadilifu katika nchi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 Katika siku hizo, naam, wakati huo, nitachipusha chipukizi mwadilifu wa uzao wa Daudi. Chipukizi huyo atatekeleza haki na uadilifu katika nchi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 “ ‘Katika siku hizo na wakati huo nitalifanya Tawi la haki lichipuke kutoka ukoo wa Daudi, naye atafanya lile lililo haki na sawa katika nchi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 “ ‘Katika siku hizo na wakati huo nitalifanya Tawi la haki lichipuke kutoka ukoo wa Daudi, naye atafanya lile lililo haki na sawa katika nchi.

Tazama sura Nakili




Yeremia 33:15
21 Marejeleo ya Msalaba  

Katika fahari yako usitawi uendelee Kwa ajili ya kweli, upole na haki Na mkono wako wa kulia Utakutendea mambo ya ajabu.


Umeipenda haki; Umeichukia dhuluma. Kwa hiyo MUNGU, Mungu wako, amekutia mafuta, Mafuta ya furaha kuliko wenzako.


Siku hiyo chipukizi la BWANA litakuwa zuri, lenye utukufu, na matunda ya nchi yatakuwa mema sana, na kupendeza, kwa ajili ya Waisraeli wale waliookoka.


BWANA akapendezwa, kwa ajili ya haki yake, kuitukuza sheria, na kuiadhimisha.


Maana alikuwa mbele zake kama mche mwororo, Na kama mzizi katika nchi kavu; Yeye hana umbo wala uzuri; Na tumwonapo hana uzuri hata tumtamani.


Mamlaka ya enzi yake yatakuzwa daima, Na kutakuwa na amani isiyo na mwisho, Katika kiti cha enzi cha Daudi na ufalme wake; Kuuthibitisha na kuutegemeza Kwa hukumu na kwa haki, Tangu sasa na hata milele. Wivu wa BWANA wa majeshi ndio utakaotenda hayo.


ndipo watakapoingia wafalme na wakuu kwa malango ya mji huu; wataketi katika kiti cha enzi cha Daudi, na kupanda magari na farasi, wao, na wakuu wao, watu wa Yuda, na wenyeji wa Yerusalemu; na mji huu utakaa hata milele.


bali watamtumikia BWANA, Mungu wao, na Daudi, mfalme wao, nitakayemwinua kwa ajili yao.


Watu wote waliowaona wamewala; na adui zao walisema, Sisi hatuna hatia, kwa kuwa hao wametenda dhambi juu ya BWANA, aliye kao la haki, yaani, BWANA, tumaini la baba zao.


Sikiliza sasa, Ee Yoshua, kuhani mkuu, wewe na wenzako wanaoketi mbele yako; maana hao ni watu walio ishara ya mambo yajayo; kwa maana, tazama, ninamleta mtumishi wangu, aitwaye Chipukizi.


Kisha nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda, aitwaye Mwaminifu na Wa kweli, naye kwa haki ahukumu na kufanya vita.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo