Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 31:28 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

28 Tena itakuwa, kwa kadiri nilivyowaangalia, ili kung'oa, na kubomoa, na kuangusha, na kuangamiza, na kutesa; kwa kadiri iyo hiyo nitawaangalia, ili kujenga, na kupanda, asema BWANA.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

28 Na kadiri nilivyokuwa mwangalifu kuwangoa, kuwabomoa, kuwaangusha, kuwaharibu na kuwatesa, ndivyo nitakavyokuwa mwangalifu kuwapanda na kuwajenga.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

28 Na kadiri nilivyokuwa mwangalifu kuwangoa, kuwabomoa, kuwaangusha, kuwaharibu na kuwatesa, ndivyo nitakavyokuwa mwangalifu kuwapanda na kuwajenga.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

28 Na kadiri nilivyokuwa mwangalifu kuwang'oa, kuwabomoa, kuwaangusha, kuwaharibu na kuwatesa, ndivyo nitakavyokuwa mwangalifu kuwapanda na kuwajenga.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

28 Kama vile nilivyowaangalia ili kung’oa na kubomoa, kuharibu, kuangamiza na kuleta maafa juu yao, vivyo hivyo nitawaangalia ili kujenga na kupanda,” asema Mwenyezi Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

28 Kama vile nilivyowaangalia ili kung’oa na kubomoa, kuharibu, kuangamiza na kuleta maafa juu yao, vivyo hivyo nitawaangalia ili kujenga na kupanda,” asema bwana.

Tazama sura Nakili




Yeremia 31:28
24 Marejeleo ya Msalaba  

Laiti ningekuwa kama nilivyokuwa katika miezi ya zamani, Kama katika siku hizo Mungu aliponilinda;


BWANA atakapokuwa ameijenga Sayuni, Atakapoonekana katika utukufu wake,


BWANA ndiye aijengaye Yerusalemu, Huwakusanya waliotawanyika wa Israeli.


Maana Mungu ataiokoa Sayuni, na kuijenga miji ya Yuda, Na watu watakaa ndani yake na kuimiliki.


angalia, nimekuweka leo juu ya mataifa na juu ya falme, ili kung'oa, na kubomoa, na kuharibu, na kuangamiza; ili kujenga na kupanda.


Ndipo BWANA akaniambia, Umeona vema, kwa maana ninaliangalia neno langu, ili nilitimize.


Kwa maana nitawaelekezea macho yangu, wapate mema, nami nitawaingiza katika nchi hii tena; nami nitawajenga, wala sitawabomoa; nitawapanda wala sitawang'oa.


Naam, nitafurahi juu yao niwatendee mema, nami nitawapanda katika nchi hii kweli kweli, kwa moyo wangu wote, na kwa roho yangu yote.


Maana BWANA asema hivi, Kama nilivyoleta mabaya haya yote makuu juu ya watu hawa, vivyo hivyo nitaleta juu yao mema hayo yote niliyowaahidi.


Ikiwa mtabaki katika nchi hii, ndipo nitawajenga, wala sitawabomoa, nami nitawapanda, wala sitawang'oa; kwa maana nayajutia mabaya niliyowatenda.


Tazama, nawaangalia niwaletee mabaya, wala si mema; nao watu wote wa Yuda, walioko hapa katika nchi ya Misri, wataangamizwa kwa upanga, na kwa njaa, hadi wakomeshwe kabisa.


Basi, mwambie hivi, BWANA asema hivi, Tazama, niliyoyajenga nitayabomoa, na niliyoyapanda nitayang'oa; na haya yatakuwa katika nchi yote.


Lakini aling'olewa kwa ghadhabu, akaangushwa chini, upepo wa mashariki ukakausha matunda yake; vijiti vyake vya nguvu vikavunjika, vikakauka; moto ulivila.


nami nitaongeza watu juu yenu, nyumba yote ya Israeli, naam, yote pia; nayo miji itakaliwa na watu, na mahali palipoharibika patajengwa.


Basi BWANA anayachungulia mabaya hayo, akatuletea; maana BWANA, Mungu wetu ni mwenye haki katika kazi zake zote azitendazo; na sisi hatukuitii sauti yake.


Basi ujue na kufahamu, ya kuwa tangu kuwekwa amri ya kutengeneza na kuujenga upya Yerusalemu hata zamani zake masihi aliye mkuu; kutakuwa na majuma saba; na katika majuma sitini na mawili utajengwa tena pamoja na njia kuu zake na handaki, naam, katika nyakati za taabu.


Siku hiyo nitaiinua tena maskani ya Daudi iliyoanguka, na kuziba mahali palipobomoka; nami nitayainua magofu yake, na kuyajenga kama siku za kale;


Nami nitawarejesha tena watu wangu Israeli waliohamishwa, nao wataijenga miji iliyoachwa maganjo, na kukaa ndani yake; nao watapanda mizabibu katika mashamba, na kunywa divai yake; nao watatengeneza bustani, na kula matunda yake.


Maana BWANA wa majeshi asema hivi, Kama vile nilivyoazimia kuwatenda ninyi mabaya, baba zenu waliponikasirisha, asema BWANA wa majeshi, wala mimi sikujuta;


vivyo hivyo nimeazimia katika siku hizi kuutendea Yerusalemu mema, na nyumba ya Yuda pia; msiogope.


Baada ya mambo haya nitarejea, Nami nitaijenga tena nyumba ya Daudi iliyoanguka. Nitajenga tena maanguko yake, Nami nitaisimamisha;


Na BWANA, Mungu wako, atakufanya uwe na wingi wa uheri katika kazi yote ya mkono wako, katika uzao wa tumbo lako, na katika uzao wa ng'ombe wako, na katika uzao wa nchi yako; kwa kuwa BWANA atafurahi tena juu yako kwa wema, kama alivyofurahi juu ya baba zako;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo