Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 31:11 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

11 Kwa maana BWANA amemweka huru Yakobo, amemkomboa mkononi mwake aliyekuwa hodari kuliko yeye.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Maana mimi Mwenyezi-Mungu nimemkomboa Yakobo, nimemwokoa kutoka kwa wenye nguvu kuliko yeye.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Maana mimi Mwenyezi-Mungu nimemkomboa Yakobo, nimemwokoa kutoka kwa wenye nguvu kuliko yeye.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Maana mimi Mwenyezi-Mungu nimemkomboa Yakobo, nimemwokoa kutoka kwa wenye nguvu kuliko yeye.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Mwenyezi Mungu atamlipia fidia Yakobo na kuwakomboa mkononi mwa walio na nguvu kuliko wao.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 Kwa kuwa bwana atamlipia fidia Yakobo na kuwakomboa mkononi mwa walio na nguvu kuliko wao.

Tazama sura Nakili




Yeremia 31:11
19 Marejeleo ya Msalaba  

Ukisikilize kilio changu, Kwa maana nimedhilika sana. Uniponye kutoka kwa wanaonifuatia, Kwa maana wao ni hodari kuliko mimi.


Hofu na woga zimewaangukia; Kwa uweza wa mkono wako wanakaa kimya kama jiwe; Hata watakapovuka watu wako, Ee BWANA, Hata watakapovuka watu wako uliowanunua.


Imbeni, enyi mbingu, maana BWANA ametenda hayo; Pigeni kelele, enyi mabonde ya nchi; Pazeni nyimbo, enyi milima; Nawe, msitu, na kila mti ndani yake. Maana BWANA amemkomboa Yakobo, Naye atajitukuza katika Israeli.


Haya, tokeni katika Babeli, Kimbieni kutoka kwa Wakaldayo; Hubirini kwa sauti ya kuimba, tangazeni haya, Yatamkeni mpaka mwisho wa dunia, semeni, BWANA amemkomboa mtumishi wake, Yakobo.


Je! Aliye hodari aweza kunyang'anywa mateka wake, au mateka wa mtu katili kuokoka?


Naam, BWANA asema hivi, Hata mateka wake aliye hodari watapokonywa mikononi mwake, na mateka wake aliye katili wataokoka; kwa maana nitapambana na yeye abishanaye nawe, nami nitawaletea wana wako wokovu.


Nao waliokombolewa na BWANA watarejea, Watafika Sayuni, wakiimba; Furaha ya milele itakuwa juu ya vichwa vyao; Watapata shangwe na furaha; Huzuni na kuugua zitakimbia.


Nami nitakuokoa kutoka kwa mkono wa watu wabaya, nami nitakukomboa kutoka kwa mkono wao wenye kutisha.


BWANA wa majeshi asema hivi, Wana wa Israeli, na wana wa Yuda wameonewa sana, na pia wana wa Yuda vivyo hivyo, watekaji wao wote wamewashikilia sana; na wamekataa kuwaachilia waondoke.


Mkombozi wao ni hodari; BWANA wa majeshi ndilo jina lake; yeye atawatetea kwa bidii, apate kuistarehesha nchi, na kuwasumbua wakaao katika Babeli.


Ee BWANA umenitetea katika kisa cha nafsi yangu; Umeukomboa uhai wangu.


Nitawakomboa kwa nguvu za kaburi; nitawaokoa kutoka kwa mauti; ewe mauti, ya wapi mapigo yako? Ewe kaburi, ku wapi kuharibu kwako? Huruma itafichika machoni mwangu.


Na BWANA, Mungu wao, atawaokoa siku hiyo, Kama kundi la watu wake; Kwa maana watakuwa kama vito vya taji, Vikimetameta juu ya nchi yake.


Ama awezaje mtu kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuviteka vyombo vyake, asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu? Ndipo atakapoiteka nyumba yake.


kama vile Mwana wa Adamu asivyokuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi.


Yesu akajibu, akawaambia, Mnapotea, kwa kuwa hamyajui maandiko wala uweza wa Mungu.


ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe na maasi yote, na kujisafishia watu wake mwenyewe walio na bidii katika matendo mema.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo