Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 30:6 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

6 Ulizeni sasa, mkaone kwamba mwanamume aona uchungu wa uzazi; mbona, basi, ninaona kila mtu anaweka mikono yake viunoni, kama mwanamke aliye na uchungu, na nyuso zote zimegeuka rangi?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

6 Jiulizeni sasa na kufahamu: Je, mwanamume aweza kujifungua mtoto? Mbona basi, namwona kila mwanamume amejishika kiunoni kama mwanamke mwenye utungu na nyuso zao zimegeuka rangi?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

6 Jiulizeni sasa na kufahamu: Je, mwanamume aweza kujifungua mtoto? Mbona basi, namwona kila mwanamume amejishika kiunoni kama mwanamke mwenye utungu na nyuso zao zimegeuka rangi?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

6 Jiulizeni sasa na kufahamu: Je, mwanamume aweza kujifungua mtoto? Mbona basi, namwona kila mwanamume amejishika kiunoni kama mwanamke mwenye utungu na nyuso zao zimegeuka rangi?

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

6 Ulizeni na mkaone: Je, mwanaume aweza kuzaa watoto? Kwa nini basi ninaona kila mwanaume mwenye nguvu ameweka mikono yake tumboni kama mwanamke aliye na uchungu wa kuzaa, kila uso ukigeuka rangi kabisa?

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

6 Ulizeni na mkaone: Je, mwanaume aweza kuzaa watoto? Kwa nini basi ninaona kila mwanaume mwenye nguvu ameweka mikono yake tumboni kama mwanamke aliye na utungu wa kuzaa, kila uso ukigeuka rangi kabisa?

Tazama sura Nakili




Yeremia 30:6
19 Marejeleo ya Msalaba  

Papo hapo tetemeko liliwashika, Uchungu kama wa mwanamke azaaye.


Kwa sababu hiyo viuno vyangu vimejaa maumivu, uchungu umenishika, kama uchungu wa mwanamke azaaye; ninaumwa sana, nisiweze kusikia; nimefadhaishwa wa hofu, nisiweze kuona.


Basi, BWANA aliyemkomboa Abrahamu asema hivi, kuhusu nyumba ya Yakobo; Yakobo hatatahayarika sasa, wala uso wake hautabadilika rangi yake.


Utasema nini wewe, atakapowaweka rafiki zako kuwa kichwa juu yako, ikiwa wewe mwenyewe umewafundisha kuwa juu yako? Je! Huzuni haitakushika, kama uchungu wa mwanamke aliye katika kuzaa?


Wewe ukaaye Lebanoni, Ujengaye kiota chako katika mierezi, Utakuwa na hali ya kuhurumiwa sana, Upatapo uchungu kama wa mwanamke azaaye.


Kwa maana nimesikia sauti, kama sauti ya mwanamke wakati wa uchungu wake, na sauti yake aumwaye, kama mwanamke azaaye mtoto wake wa kwanza, sauti ya binti Sayuni, atwetaye kupata pumzi, na kunyosha mikono yake, akisema, Ole wangu, sasa! Kwa maana roho yangu inazimia mbele ya wauaji.


Miji imetwaliwa, ngome zimeshambuliwa, na mioyo ya mashujaa wa Moabu siku hiyo itakuwa kama moyo wa mwanamke akiwa katika uchungu wa kujifungua.


Tazama, atapanda na kuruka kama tai, na kutandaza mabawa yake juu ya Bozra; na mioyo ya mashujaa wa Edomu siku hiyo itakuwa kama moyo wa mwanamke akiwa katika uchungu wa kujifungua.


Dameski umedhoofika; Umejigeuza kukimbia; tetemeko limeushika; Dhiki na huzuni zimeupata, Kama za mwanamke katika uchungu wake.


Mfalme wa Babeli amesikia habari zao, Na mikono yake imekuwa dhaifu; Dhiki imemshika, na maumivu, Kama ya mwanamke akiwa katika uchungu wa kujifungua.


Tumesikia habari zake; mikono yetu inalegea; dhiki imetushika, na uchungu kama wa mwanamke wakati wa kuzaa kwake.


Ndipo uso wa mfalme ukambadilika; fikira zake zikamfadhaisha; viungo vya viuno vyake vikalegea; magoti yake yakagongana.


Uchungu wa mwanamke mwenye mimba utampata; yeye ni mwana asiye na akili; maana wakati umewadia, ambao haimpasi kukawia mahali wapenyapo watoto.


Mbele yao watu wanahangaika; nyuso zote zimegeuka kuwa nyeupe kwa hofu.


Amekuwa utupu, na ukiwa, na uharibifu; hata moyo unayeyuka, na magoti yanagonganagongana; moyoni kote mna uchungu, na nyuso za wote zimekuwa nyeupe kwa hofu.


Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafla, kama vile uchungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo