Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 30:20 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

20 Watoto wao nao watakuwa kama zamani, na kusanyiko lao litathibitika mbele zangu, nami nitawaadhibu wote wanaowaonea.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

20 Watoto wao watakuwa kama walivyokuwa zamani, jumuiya yao itaimarika mbele yangu, nami nitawaadhibu wote wanaowakandamiza.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

20 Watoto wao watakuwa kama walivyokuwa zamani, jumuiya yao itaimarika mbele yangu, nami nitawaadhibu wote wanaowakandamiza.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

20 Watoto wao watakuwa kama walivyokuwa zamani, jumuiya yao itaimarika mbele yangu, nami nitawaadhibu wote wanaowakandamiza.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

20 Watoto wao watakuwa kama walivyokuwa siku za zamani, nayo jumuiya yao itaimarishwa mbele yangu; nitawaadhibu wote wanaowadhulumu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

20 Watoto wao watakuwa kama walivyokuwa siku za zamani, nayo jumuiya yao itaimarishwa mbele yangu; nitawaadhibu wale wote wawaoneao.

Tazama sura Nakili




Yeremia 30:20
16 Marejeleo ya Msalaba  

Kizazi kitakachokuja kitaandikiwa hayo, Na watu watakaoumbwa watamsifu BWANA.


Wana wa watumishi wako watakaa, Na wazawa wao wataimarishwa mbele zako.


Na hao wanaokuonea nitawalisha nyama yao wenyewe, nao watalewa kwa kuinywa damu yao wenyewe, kama kwa mvinyo mpya; na watu wote watajua ya kuwa mimi, BWANA, ni mwokozi wako, na Mkombozi wako ni Mwenye enzi wa Yakobo.


BWANA, Bwana wako na Mungu wako, awateteaye watu wake, asema hivi, Tazama, nimeondoa mkononi mwako kikombe cha kulevyalevya, hilo bakuli la hasira yangu; hutalinywea tena;


Utathibitika katika haki; utakuwa mbali na kuonewa, kwa maana hutaogopa; na mbali na hofu, kwa maana haitakukaribia.


Israeli walikuwa utakatifu kwa BWANA; malimbuko ya uzao wake; Wote watakaomla watakuwa na hatia; uovu utawajia; asema BWANA.


Basi, watu wote wakulao wataliwa; na adui zako wote watakwenda kufungwa; kila mmoja wao; na hao waliokuteka nyara watatekwa; na wote waliokuwinda nitawafanya kuwa mawindo.


nami nitawapa moyo mmoja na njia moja, wapate kunicha sikuzote; kwa mema yao, na ya watoto wao baada yao;


Ee BWANA, utugeuze kwako, nasi tutageuka; Zifanye mpya siku zetu kama siku za kale.


Nami nitaitia nguvu nyumba ya Yuda, nami nitaiokoa nyumba ya Yusufu, nami nitawarudisha, kwa maana nawaonea rehema; nao watakuwa kana kwamba sikuwatupa; kwa maana mimi ni BWANA, Mungu wao, nami nitawasikia.


Nitawapigia kelele, na kuwakusanya pamoja; kwa maana nimewakomboa; nao wataongezeka kama walivyokua hapo awali.


Na hizo njia za mji zitajaa wavulana, na wasichana, wakicheza katika njia zake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo